• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 25, 2012

  KUZIONA SIMBA NA AL AHLY BUKU TANO TU              TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  NDUGU waandishi.

  Kama mnavyofahamu, Jumapili ya Aprili 29 mwaka huu, timu ya soka ya Simba inakutana na klabu ya Al Ahly Shandy kutokaSudan katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF), kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
  Simba ni timu pekee kutoka katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyobaki katika michuano yote ya kimataifa inayosimamiwa na CAF. 
  Kubwa zaidi, ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania waliobaki katika michuano ya kimataifa na hivyo wanabeba bendera ya taifa kokote kule waliko. 
  Maandalizi yote kwa ajili ya pambano hilo yamekamilika. 
  Wapinzani wetu, Al Ahly wanatarajiwa kuwasili kesho saa saba mchana kwa ndege ya Ethiopia Airlines. 
  Waamuzi na Kamishina wa mchezo wamepangwa kuwasili Ijumaa (keshokutwa) wakitokea nchini Swaziland na Rwanda.

  VIINGILIO 
  Kutokana na ukweli kwamba mechi hiyo itakuwa ya kimataifa, Simba imepanga viingilio ambavyo kila mwananchi ataweza kuvimudu. Viingilio vitakuwa kama ifuatavyo. 
  Viti vya bluu na kijani itakuwa Sh. 5,000, Rangi ya Chungwa Sh, 10,000, VIP C 15,000, VIP B 20,000 na VIP A 30,000. 
  Tiketi zitauzwa katika maeneo yafuatayo, Big Bon, Benjamin Mkapa, Stears Mjini, Mbagala Dar Live, OilCom Buguruni, Tandika Mwembeyanga, Ubungo Oilcom, Mwenge Bus Stand, BP Mwananyamala na Gapco Ukonga. 
  Tiketi zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa asubuhi katika maeneo yaliyotajwa. 
  Klabu imepokea maombi mengi kutoka kwa wanachama na wapenzi wake kutoka mikoani na ingeomba kwamba wale wanaotaka kuja kutazama mechi hii kwa makundi kutoka mikoani, wawasiliane mapema na uongozi ili wanunuliwe tiketi zao mapema.
   Simba SC imechapa tiketi za kutosha na ingeomba wapenzi na wanachama wake kujitokeza kwa wingi kwenye pambanohilo. 
  Wana Simba wote wanaombwa kuja uwanjani wakiwa wamevalia mavazi yao ya rangi Nyekundu na Nyeupe ili uwanja mzima upendeze kwa rangi hizo. 
  Tunatoa wito kwa vyombo vya habari kuisaidia Simba naTanzania kwa kuelekeza nguvu zao katika uandishi wa taarifa ambazo zitaisaidia timu yetu kusonga mbele na si kuondoa morali au kusababisha watu wasiende uwanjani.

  Shukrani. 
  Uongozi wa Simba SC unatoa shukrani, kwa namna ya kipekee kabisa, kwa serikali kutokana na uamuzi wake wa kuruhusu Wekundu wa Msimbazi kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa kujiandaa na mechi hii muhimu. 
  Ezekiel Kamwaga
  Msemaji
  Simba SC


  SOURCE: mamapipiro.blogspot.com
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KUZIONA SIMBA NA AL AHLY BUKU TANO TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top