• HABARI MPYA

  Sunday, April 29, 2012

  AMINIA MNYAMA SIMBA SC, LAZIMA MTU AKAE

  Kikosi cha kwanza cha Simba SC

  Makala

  Simba hakuna lisilowezekana
  Imeandikwa na Clecence Kunambi; Tarehe: 27th April 2012 @ 14:30 Imesomwa na watu: 67; Jumla ya maoni: 0

      
  Habari Zaidi:
 • Ratiba Ligi Kuu inatoa mwanya upangaji matokeo
 • Gabriel Zacharia ajivunia kumuibua Ulimwengu
 • Madhara ya chumvi kupita kiasi kwa wanamichezo
 • Simba hakuna lisilowezekana
 • Salma,bondia chipukizi Moro anayekuja juu
 • Semeni:Nyota Twiga Stars mwenye vipaji kibao
 • Rais Bingu wa Mutharika alijitabiria kifo
 • Amini awakunia kichwa mashabiki wake
 • Mabondia kuvuna walichopanda Morocco
 • Hope Vicoba kimbieni mithili ya pundamilia
 • Utamaduni na historia vyaweza kukuza utalii nchini
 • Wapare,kabila lenye mafundisho yanayofaa kuigwa Tanzania
 • CCM, CUF: Muungano ni lulu ya Tanzania
 • Muungano wa Tanzania una historia ndefu, hauvunjiki
 • Kasoro za Muungano zisiwe kigezo cha kuvuunja
 • Mjadala wa mafuta usitishie uhai wa Muungano
 • Balozi Karume, mwakilishi wa marais wote wa Tanzania
 • Tatizo la maji Geita sasa basi
 • Ewura yaongeza pato la taifa kupitia XRF
 • Wafanyabiashara soko la Bonanza watoa ya moyoni

 • Habari zinazosomwa zaidi:
 • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
 • Balaa lingine kwa Chenge
 • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
 • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
 • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
 • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
 • Vatican yamvua jimbo Askofu
 • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
 • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
 • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
 • NI karata muhimu kwa wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa Simba pale itakapoikaribisha timu ya Al Ahly Shandy ya Sudan kwenye mchezo wa kwanza wa raundi
  ya tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

  Mpaka kufikia hatua hiyo Simba imeziondoa mashindanoni timu za Kiyovu ya Rwanda na Entente Setif ya Algeria na kesho inacheza dhidi ya timu hiyo kutoka Sudan na kama itaiondoa mashindanoni itabakiwa na raundi moja kuingia kwenye makundi.

  Al Ahly Shandy sio miongoni mwa timu mbili kubwa za Sudan lakini uwepo wa timu hiyo kwenye mashindano hayo sio kitu cha kubeza, kwani ni bora na ndio maana ipo na imefikia hatua hiyo ya mashindano hayo.

  Simba imekuwa ikicheza vizuri na kwa mbinu kubwa kwenye hatua zote za mashindano hayo, ukianzia mechi ya kwanza dhidi ya Kiyovu mpaka iliyopita dhidi ya Setif na kutokana na kuimarika vizuri kwa timu hiyo kiufundi na kimbinu ndio maana imefika hapo ilipo.

  Ilianza ugenini dhidi ya Kiyovu ikafanikiwa kupata bao la ugenini katika sare ya bao 1-1 pale Kigali Rwanda, Simba walitangulia kufunga kwa bao la Mwinyi Kazimoto na Wanyarwanda hao kusawazisha.

  Kwa kanuni za CAF bao moja la ugenini huhesabiwa kama mabao mawili hivyo ni kamaSimba ilishinda kwa mabao 2-1 Kigali na kuhitaji sare ama ushindi wa aina yoyote kusonga mbele.

  Waliporudiana na timu hiyo kwenye Uwanja wa Taifa Simba chini ya kocha Milovan Cirkovic
  haikutaka kucheza kwa kutafuta sare bali kupata mabao ya haraka haraka yatakayoihakikishia
  kusonga mbele, ikafunga mabao mawili ya haraka haraka na hata jamaa wa Kiyovu walipokumbuka shuka kwa bao moja la dakika za mwisho kulikuwa kulishakucha.

  Kwa staili hiyo ikavuka na safari hii ikapangwa kuanzia nyumbani dhidi ya timu hiyo kutoka Algeria, ambayo nayo ilijitahidi kucheza soka la ugenini kwa kumsimamisha mshambuliaji mmoja mbele na kujaza viungo wengi katikati ya uwanja.

  Mfumo huo ulionekana kuichanganya sana Simba hasa kipindi cha kwanza kwani walienda mapumziko wakiwa hawajafungana, lakini kikosi hicho Milovan kilibadilika kipindi cha pili kwa kucheza mpira wa kasi huku ikiwatumia vyema wachezaji wake wenye kasi Emmanuel Okwi na Salumu Machaku kuufungua msitu wa waarabu uliojazana golini kwao.

  Ndipo wakapata mabao mawili ya Haruna Moshi na Okwi lakini huku ikicheza kwa tahadhari kubwa kuizuia Setif isipate hata bao, kwani baada ya Simba kupata mabao yao mawili Setif waliacha mbinu zao chafu za kupaki basi na kuamua kucheza mpira.

  Na walipokwenda Algeria mbali na kucheza pungufu kwa muda mrefu baada ya beki Juma
  Nyosso kuoneshwa kadi nyekundu bado walijituma na kutoruhusu zaidi ya mabao matatu na kwa kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kutumia uwezo binafsi wa Okwi wakapata bao lililowavusha kwenye hatua hii.

  Ukifuatilia Simba kwa sasa mbali na uwezo wa wachezaji kama Okwi, Haruna Moshi na Patrick Mafisango kuonekana wa kipekee kutokana na vipaji walivyojaliwa nyota hao na Mwenyezi Mungu lakini wachezaji wengine wote wa ndani ni wa kawaida ila waliounganishwa vyema
  kitimu.

  Simba inacheza kitimu sana na inapata mabao yake kwa mfumo unaoeleweka kwa lugha ya soka unaweza kuita mabao ya ‘Move’ yanayotengenezwa vizuri na mawinga wa timu hiyo Okwi, Uhuru Selemani ama Salumu Machaku, ambao wanapokea mipira toka kwa viungo wake Haruna Moshi, Patrick Mafisango na Mwinyi Kazimoto.

  Kinachopaswa kufanywa na wekundu hao wa Msimbazi ni kama walichofanya katika mechi dhidi ya Setif kutafuta mabao mengi kwa kadiri itakavyowezekana kwenye mechi ya kesho ili wawe na wakati mzuri kwenye mechi ya marudiano huko Sudan.

  Al Ahly Shandy sio timu ya kubeza kwani inaundwa na nyota wengi waliokuwa wakisugua
  benchi kwenye timu za El Hilal na El Merreikh, hivyo ni wazi uzoefu walioupata kutoka kwa miamba hiyo kihistoria ya Sudan unaweza ukaisumbua Simba kama wasipokuwa makini.

  Wacheze soka la kasi na kutumia kila nafasi yatakayoipata huku wakitilia maanani kuwa kwenye mechi za kimataifa huwa hazipatikana nafasi nyingi sana kutokana na umakini wa timu zenyewe, wakishindwa kuzitumia lazima wajue kuwa itawagharimu.

  Kitu kingine ni kuwa na nidhamu kubwa muda wote wa mechi hiyo waepuke kufanya makosa yatakayowafanya wapate kadi nyekundu hao hata za njano zitakazowafanya kukosa mchezo wa marudiano kwani timu kutoka Uarabuni huwa zinacheza sana na marefa.

  Hakuna sababu labda mtu fulani awaambie hivyo wao wenyewe kwani wengi wao ni wachezaji wa kimataifa wanafahamu fika gharama za kucheza wakiwa pungufu uwanjani, hivyo nidhamu inapaswa kuwa ya hali ya juu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMINIA MNYAMA SIMBA SC, LAZIMA MTU AKAE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top