• HABARI MPYA

  Monday, April 30, 2012

  YANGA-MBIWA ABISHA HODI MAN UNITED, ASEMA HATA ARSENAL POA


  Mapou Yangambiwa - Montpellier (Panoramic) (Portrait only)
  NAHODHA wa Montpellier ya Ufaransa, Mapou Yanga-Mbiwa amesema ndoto yake ni kucheza Manchester United.

  Kinda huyo wa miaka 22, ameibeba Montpellier kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya Ufaransa msimu huu na amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Newcastle United na Bayern Munich.

  Yanga-Mbiwa pia amezungumzia jinsi anavyovutiwa na kuhamia Arsenal mwishoni mwa msimu.

  Beki huyo wa kati mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2013 na alijiunga na La Paillade mwaka 2006, akianzia timu ya vijana na tangu wakati huo amekuwa lulu kwenye klabu hiyo .
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA-MBIWA ABISHA HODI MAN UNITED, ASEMA HATA ARSENAL POA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top