• HABARI MPYA

    Wednesday, April 18, 2012

    NEVILLE AMUONGEZA 'MASIKA' GIGGS UNITED

    
    Giggs
    BEKI mstaafu wa England, Gary Neville amemkingia kifua mchezaji mwenzake wa zamani kwa muda mrefu, Manchester United, Ryan Giggs kuendelea kucheza hadi akiwa ana umri wa miaka 40, kwa sababu ana uwezo wa kufanya mambo makuvwa Old Trafford kwa muda mrefu.
    Beki huyo wa zamani wa pembeni wa England, alistaafu katikati ya msimu uliopita na kuwa mchambuzi kwenye vyombo vya habari, baada ya kushinda mataji kadhaa na United.
    Wote, Neville na Giggs walikuwa kwenye timu ya vijana ya United, iliyoitwa mwaka 1992, ambayo ilitoa wachezaji kibao wa kupandisha timu ya wakubwa Old Trafford.
    Lakini winga huyo wa Wales aliyehamia nafasi ya kiungo, Giggs kwa kiasi kikubwa alikuwa akipewa heshima ya nyota zaidi kwenye kikosi hicho na akiwa na umri wa miaka 38, hivi sasa anaweza kukuza rekodi yake ya kuchukua mataji ya Ligi Kuu England hadi 13 iwapo watatwaa ubingwa na msimu huu.
    Kocha wa United, Sir Alex Ferguson tayari amemtaka Giggs kusaini mkataba wa msimu mmoja zaidi, lakini Neville amesema ana nafasi ya kucheza kwa misimu zaidi.
    "Tutamuona kama yeye tena? Hapana, hakuna njia," alisema Neville.
    "Ryan Giggs anaweza kuwa mwansoka mwenye mafanikio zaidi daima Uingereza na siwezi kumuona yeyote anayeweza kumpiku,”alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NEVILLE AMUONGEZA 'MASIKA' GIGGS UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top