• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 27, 2012

  SIMBA SC, AL AHLY NGOMA INOGILE


  Kikosi cha Simba
  MAKOCHA wa timu za Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan kesho (Aprili 28 mwaka huu) watakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari kuzungumzia walivyoandaa vikosi vyao kwa ajili ya mechi ya Jumapili.
  Itakuwa ni mechi ya kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.
  Mkutano huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
  Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho itachezwa Uwanja wa Taifa kuanzia saa 10 kamili jioni.
  Simba imefika hatua hii, baada ya kuitoa ES Setif ya Algeria, wakati Al Ahly Shandy imeitoa Ferroviario ya Msumbiji.
  Timu hizo zitarudiana wiki mbili zijazo Sudan na mshindi wa matokeo ya jumla ataingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC, AL AHLY NGOMA INOGILE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top