MABAO matatu ya Luis Suarez (hat-trick), likiwemo lile kali alilofunga kutoka umbali wa mita 45, yameisaidia Liverpool kuifunga Norwich katika Ligi Kuu ya England usiku huu, wakijiandaa kuingia kwenye fainali ya Kombe la FA.
Liverpool imefikisha pointi 49, ikiwa nafasi ya nane baada ya kucheza mechi 35, inazidiwa pointi mbili na Everton iliyo nafasi ya saba.