• HABARI MPYA

    Tuesday, April 24, 2012

    KASEBA, CHEKA KURUDIANA JULAI 7 DAR


    Kaseba kulia akisaini kuzipiga na Cheka. Kushoto ni promota Kaike Siraju

    BINGWA wa zamani wa Kick Boxing, Japhet Kaseba amesaini mkataba wa kucheza na Bingwa wa dunia wa ndondi wa IBC, Francis Cheka wa Morogoro katika pambano la uzito wa Middle, Julai 7, mwaka huu Dar es Salaam
    Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Kaseba amesema anashukuru kupata mpambano huo na atahakikisha anaonyesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mapambano
    “Najua mabondia wa hapa bongo wananikwepa sana kwa kuwa nimeshakuwa bingwa wa ngumi za mateke, lakini hawajui mimi ni bingwa katika mapigano yote,” alisema Kaseba.
    “Nitahakikisha naweka kambi ya kutosha na kukata ngebe za Cheka, ni mtoto mdogo sana katika masumbwi kwa kweli bingwa wa kweli ni Rashid Matumla ambaye ninamuheshimu, mpaka sasa Cheka kanikimbia muda mrefu tu tangu tupambane mara ya kwanza (Oktoba 3, 2009),”alisema Kaseba.
    Cheka alishinda pambano la kwanza kwa Technical Knockout (TKO), lakini Kaseba anadai alipewa ubingwa kwa kusingizia mashabiki wake walimtupa nje ya ulingo.
    “Kazi yake yeye anarudiana na Mada Maugo kila siku, lakini kwa sasa kakanyaga miwaya zamu yake imefika,”alisema.
    Naye Promota wa mpambano huo, Kaike Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam katika ukumbi ambao mutatajwa baadaye.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KASEBA, CHEKA KURUDIANA JULAI 7 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top