• HABARI MPYA

  Friday, April 27, 2012

  GUARDIOLA AAGA RASMI BARCA, TITO APEWA MIKOBA YAKE


  Tito Vilanova, Barcelona
  Tito
  KLABU ya Barcelona imethibitisha kwamba Tito Vilanova atakuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo mwishoni mwa msimu Pep Guardiola atakapoondoka.
  Kocha huyo kijana mwenye umri wa miaka 42 amekuwa Kocha Msaidizi Camp Nou tangu Guardiola aanze kazi mwaka 2008, na amekuwa nyuma ya mafanikio ya Pep ya kuiwezesha klabu kutwaa mataji 13 ndani ya miaka minne.

  Aliwaambis Waandishi: "Nakushukuru, Pep, kwa furaha yote uliyotuletea na kutuletea soka ya kisasa ambayo haina swali."

  NI SAHIHI KUONDOKA KWA GUARDIOLA?
  5/1Pep Guardiola anakwenda wapi sasa, Manchester City?
  Kutajwa haraka kwa Vilanova baada ya kijiuzulu kwa Mspanyola huyo leo mchana hakukutarajiwa, huku Laurent Blanc, Marcelo Bielsa na Ernesto Valverde waliotarajiwa kupewa kazi wakiambulia patupu.

  Mechi ya mwisho ya Guardiola kuiongoza  Blaugrana itakuwa Mei 25, wakati Barcelona itakapomenyana jna Athletic Bilbao kwenye fainali ya Kombe la Mfalme.
  Hatua ya kuachia ngazi Barca, inafuatia timu hiyo kuvuliwa ubingwa wa Ulaya na Chelsea katika Nusu Fainali ya michuano hiyo, wakilazimishwa sare ya 2-2 na The Blues waliocheza 10, kutokana na John Terry kupewa kadi nyekundu mapema kipindi cha kwanza .

  Kabla ya mechi hiyo ya Nusu fainali, mabingwa hao watetezi wa La Liga walifungwa 2-1 na Real Madrid Uwanja wao wa Camp Nou katika ligi hiyo kuu ya Hispania na kupoteza matumaini ya kutetea taji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GUARDIOLA AAGA RASMI BARCA, TITO APEWA MIKOBA YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top