• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 30, 2012

  MESSI AMFIKIA ROLANDO KWA MABAO LA LIGA


  Leo Messi celebrando con el FC Barcelona
  Getty Images
  MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi jana alirejesha makali yake ya kupachika mabao alipofunga mawili wakati Barcelona ikiikung'uta 7-0 Rayo Vallecano na kumfikia Cristiano Ronaldo kwa mabao 43 kwenye Ligi Kuu ya Hispania msimu huu, wawili huo wakizidi kukabana koo katika kuwania kiatu cha dhahabu Ulaya.

  Nyota wa Ureno, pia alifunga mabao mwishoni mwa wiki baada ya kufunga bao la kuongoza katika ushindi wa Real Madrid wa 3-0 dhidi ya Sevilla Uwanja wa Santiago Bernabeu.

  Anayewafuatia kwa pointi 30 Ronaldo na Messi ni Robin van Persie, ambaye amekaribia mabao 30 baada ya kufunga bao la kusawazisha Arsenal ikitoka 1-1 ugenini na Stoke Jumamosi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI AMFIKIA ROLANDO KWA MABAO LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top