• HABARI MPYA

    Friday, April 27, 2012

    LALA SALAMA LIGI KUU YAELEKEA UKINGONI


    Bobana wa Simba katika moja ya mechi za Ligi Kuu

    LIGI Kuu ya Vodacom Tanazania Bara inaendelea katika raundi ya 25 kesho (Aprili 28 mwaka huu) ambapo Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa mgeni wa African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi.
    Aprili 30 mwaka huu Azam na Toto African zitacheza Chamazi wakati Mei 1 mwaka huu Villa Squad itaumana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Chamazi.
    Ligi hiyo itafunga msimu wa 2011/2012, Mei 5 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa uwanjani. Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha) na Ruvu Shooting vs Villa Squad (Mabatini, Mlandizi).
    Mechi nyingine zitakuwa kati ya Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani, Tanga), African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu, Morogoro), Azam vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es Salaam) na Moro United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LALA SALAMA LIGI KUU YAELEKEA UKINGONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top