• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 24, 2012

  CHINA ASIKITIKIA SOKA YA TANZANIA


  China kushoto akiwa BIN ZUBEIRY kulia

  KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Athumani Abdallah China amesema kwamba anasikitika jinsi ambavyo soka ya Tanzania inazidi kuporomoka, wakati haoni jitihada za kuikwamua.
  “Hali ya sasa inasikitisha, naambiwa sasa hata wachezaji wa nafasi ya kiungo ni tabu, yaani watoto wa siku hizi sijui wanafanya nini.
  Nadhani ni starehe sana, hawana mazoezi. Hawawezi kucheza mpira namna hii, na hii ni kwa sababu hakuna misngi mizuri. Wachezaji hawajitambui na hawana malengo, wanacheza tu basi,”alisema China.
  China anayeishi London, Uingereza yupo nchini kwa muda kwa ajili ya masuala ya kifamilia tangu juzi na anatarajiwa kuondoka Jumapili.  
  Kiungo huyo wa zamani wa Yanga na Simba SC, alisema kwamba kazi kubwa lazima ifanyike ili soka ya Tanzania irudi kwenye heshima yake, vinginevyo hali itazidi kuwa mbaya zaidi.
  “Tuna bahati tuna rais anayependa michezo, lakini tumeshindwa kumtumia.  Nafasi hii tutaijutia sana, akiondoka huyu (Jakaya Kikwete) kumpata rais mwingine mpenda michezo kama yeye, itachukua muda sana,”alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHINA ASIKITIKIA SOKA YA TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top