• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 27, 2012

  LIGI KUU ZANZIBAR YAPATA UDHAMINI


  GRAND MALT MDHAMINI MPYA LIGI KUU ZANZIBAR


  CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), leo kinatarajia kusaini mkataba wa udhamini wa Ligi Kuu ya Zanzibar na kampuni inayotengeneza kinywaji cha Grand Malt.
  Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa ZFA, Munir Zakaria, utiaji saini mkataba huo wa miaka mitatu, ni faraja kubwa kwa klabu 12 za ligi hiyo  baada ya kujiondoa kwa Kampuni ya Usafirishaji wa Baharini ya Seagull mapema mwaka uliopita kutokana na sababu za kiuendeshaji.
  Munir, alisema, ZFA ikiwa ndiyo mlezi wa klabu za soka, imefarijika kutokana na kujitokeza kwa mdhamini huyo ambaye ameahidi kurudisha ushindani wa ligi hiyo masikini visiwani hapa.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari, Grand Malt itadhamini ligi ya msimu ujao utakaoanza Agosti kwa thamani ya shilingi milioni 140.
  Munir alisema, klabu zinatarajiwa kupatiwa kiasi cha shilingi milioni nane kila moja zikiwemo fedha za usafiri pamoja na mahitaji mengine ya kujikimu kwa ajili ya vyakula na malazi wakati zitakapokuwa kwenye vituo Unguja na Pemba.

  SOURCE: mamapipiro.blogspot.com
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIGI KUU ZANZIBAR YAPATA UDHAMINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top