• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 26, 2012

  MOURINHO AWAPA UBINGWA CHESLEA


   26 Aprili, 2012 - Saa 11:53 GMT
  Jose Mourinho
  Meneja wa zamani wa Chelsea anasema angelipenda kuona Chelsea wakiibuka washindi katika fainali dhidi ya Bayern Munich
  KOCHA Jose Mourinho wa Real Madrid ya Hispania, amesema angelipenda Chelsea ya England ipate ushindi itakapocheza na Bayern Munich katika mechi ya fainali ya soka ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mjini Munich mwezi ujao.
  Mourinho amesema hayo baada ya Real kushindwa na timu ya Bayern Munich ya Ujerumani kupitia mikwaju ya penalti.
  Chelsea walifuzu kuingia fainali baada ya kuishinda Barcelona, pia ya Uhispania, na kwa muda mrefu wakicheza wakiwa 10.
  "Bila shaka ningelipenda Chelsea wawe washindi. Walikuwa ni mashujaa kuishinda Barcelona wakiwa na wanaume kumi uwanjani," alisema meneja huyo wa zamani wa The Blues.
  "Mimi ninajivunia wachezaji wangu, lakini katika mechi kubwa kama hiyo, tulihitaji nguvu zaidi na tulipaswa kuwa wachangamfu."
  Kutokana na wachezaji wa timu zote kufanya makosa ambayo ililazimika mwamuzi kuwaadhibu katika mechi za nusu fainali, Bayern Munich na Chelsea zote zitawakosa wachezaji mahiri.
  Bayern itazikosa huduma za David Alaba, Holger Badstuber na Luiz Gustavo.
  Chelsea nayo itacheza pasipo Ramires, John Terry, Branislav Ivanovic na Raul Meireles kuingia uwanjani.
  Lakini licha ya Real kuanza kwa kasi, na hasa baada ya kuwashinda wapinzani wao wakuu Barca katika ligi kuu ya nyumbani ya La Liga mwishoni mwa wiki, walishindwa kupata bao la ushindi dhidi ya Bayer, ambyo iliweza kuwatumia wachezaji waliokuwa wamepata nafasi ya kupumzika, baada ya ubingwa wa Bundesliga kuchukuliwa na Borussia Dortmund.
  "Lazima uweze kuwa katika hali ya wastani, iwapo utashinda au utashindwa," Mourinho alisema.
  "Vijana walicheza vizuri, na kiakili wakiwa imara, na wakitambua walikuwa wanacheza na timu kali, na timu ambayo mwishoni mwa wiki iliyopita ilikuwa likizoni.
  "Tulishindwa, tunahuzunika, na wao wamefurahi, lakini hiyo ndio hali ya kandanda."

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MOURINHO AWAPA UBINGWA CHESLEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top