
David Obua akichzea Uganda Cranes
MWANASOKA wa kimataifa wa Uganda, David Obua anaelekea kuihama klabu yake, Hearts ya huko Scotland baada ya kuarifiwa kuwa hataongezewa mkataba mwishoni mwa msimu huu.
Mcheza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, aliyehamia Scotlanda kutoka klabu ya Kaizer chiefs ya Afrika ya kusini mwezi julai mwaka 2008, ameichezea klabu ya Hearts mara 100 katika kipindi cha miaka minne.
Lakini toka mwezi Febuari hajashiriki mechi na msemaji wa Hearts amesema kwenye tovuti ya klabu hio kua ''Tungependa kumshukuru David kwa huduma yake na mchango wakati wote alioichezea klabu hii na tunamtakia kila la heri.
0 comments:
Post a Comment