• HABARI MPYA

  Sunday, April 29, 2012

  SOUTHAMPTON YAREJEA LIGI KUU ENGLAND


   28 Aprili, 2012 - Saa 15:23 GMT
  Southampton
  Southampton imerudi tena katika ligi kuu ya Premier ya England baada ya kutokuwepo miaka saba
  KLABU ya Southampton imepanda Ligi Kuu ya England, baada ya jana (Jumamosi) kuifunga Coventry mabao 4-0.
  Southampton ilikuwa katika uwanja wa nyumbani wa Mt. Mary.
  Magoli yalikuwa ni kutoka kwa Billy Sharp, Jose Fonte, Jose Hooiveld na Adam Lallana.
  Southampton inarudi tena katika ligi kuu ya Premier baada ya kutokuwepo kwa miaka saba.
  Coventry, ambao tayari wameshukishwa hadhi, walifungwa kwa urahisi na timu ya Southampton ikiwa nyumbani, na kutokana ushindi wake, inamaanisha West Ham, sasa wamesukumwa nyuma hadi nafasi ya tatu katika ligi hiyo ya Championship.
  Miaka saba iliyopita, Southampton iliondolewa kutoka ligi kuu ya Premier, lakini kutokana na marehemu Marcus Liebher, aliyekuwa akimiliki klabu, pamoja na mwenyekiti Nicola Cortese, waliweza kuwekeza zaidi katika timu na kuifanya thabiti.
  Juhudi zao hatimaye zimeiwezesha Southampton kurudi katika ligi kuu ya Premier.
  Kampeni ya Southampton hasa imenufaika sana kutokana na mabao 31 msimu huu ya mshambulizi Rickie Lambert, lakini mchango wa kiungo cha kati Lallana pia umekuwa muhimu sana.
  Wachezaji Rickie Lambert na Billy Sharp wanatazamiwa kung'ara katika ligi kuu ya Premier msimu ujao.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SOUTHAMPTON YAREJEA LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top