• HABARI MPYA

  Thursday, April 26, 2012

  VIBONDE WATARAJIWA WA SIMBA WATUA DAR


  Thursday, April 26, 2012

  AL AHLY SHANDY WATUA, SUMAYE MGENI RASMI

  WAKATI msafara wa watu 30 wakiwemo wachezaji na viongozi wa timu ya soka ya Al Ahly Shandy ya Sudan ukiwasili nchini leo kwa ajili ya kukwaana na Simba, mgeni rasmi katika mechi hiyo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.  
  Timu hizo zitakwaana Aprili 29 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa 16 bora ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF).
  Akizungumza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Kimataifa wa Mwl. JK Nyerere, kocha mkuu wa Al Ahly Kouk Mohammed aliiambia mamapipiro blog kwamba mchezo huo uantarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwani Simba ni timu nzuri.
  Alisema anaifahamu Simba kama moja ya timu mahiri barani Afrika sambamba na kuwa na uzoefu wa kucheza michuano ya kimataifa hali ambayo itawafanya wawe makini zaidi pindi watakaposhuka dimbani.
  Hata hivyo kocha huyo raia wa Tunisia alisema kwamba huenda wakaathiri kidogo na hali ya hewa ya Tanzania kutokana na kuwa tofauti na Sudan ingawa watajitahidi kukabiliana nayo.
  Kikosi cha Al Ahly kinaundwa na wachezaji watano wa kimataifa wakiwemo wawili kutoka Nigeria , mmoja kutoka Mali na mwingine kutoka Mali huku wachezaji wawili wakiichezea timu ya Taifa ya Sudan .
  Al Ahly wanakutana na Simba baada ya kuitoa Ferroviario ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 3-0, huku Simba iliitoa Es Setif ya Algeria huku Simba ikibebwa na bao la ugenini baada ya nyumbani kushinda 2-0 kabla ya kwenda kufungwa 3-1.
  Katika hatua nyingine tiketi kwa ajili ya kushuhudia mpambano huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo katika vituo tofauti jijini Dar es salaam huku waamuzi wa mchezo huo kutoka Swaziland Nhleko Simanga Pritchard, Mbingo Petros Mzikayifani,Sibandze Thulani, Fakudze Mbongiseni Elliot na Kamishna wa Kayijuga Gaspard wa Rwanda wanatarajiwa kuwasili leo.
  Katika kujiandaa na mchezo huo, Simba imepiga kambi eneo la Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam ambapo kocha mkuu wa Simba Mserbia Milovan Cirkovic amejinasibu kushinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki mbili zijazo katika jiji la Shandy , Sudan .

  SOURCE: mamapipiro.blogspot.com
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VIBONDE WATARAJIWA WA SIMBA WATUA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top