• HABARI MPYA

    Monday, April 30, 2012

    MNYAMA AENDA ZENJI KUKUSANYA NGUVU ZA KUCHANA KANDAMBILI


    SIMBA HAOOOOO ZENJI, YANGA WAJICHIMBIA KLABUNI


    HOMA ya mpambano wa ligi kuu bara baina ya watani wa jadi nchini Simba na Yanga imeanza kupanda ambapo leo timu hizo zimeingia kambi kujiandaa na mpambano wao utakaopigwa Mei 5 kwenye dimba la taifa. 
    Wakati Yanga ikiingia kambini katika hosteli zilizopo klabuni kwao mitaa ya Jangwani na Twiga, Simba wameelekea Visiwani Zanzibar ambapo mara nyingi huenda kujiandaa na michezo muhimu ikiwemo dhidi ya Yanga. 
    Habari ambazo mamapipiro blog imezipata jijini Dar es Salaam, zinaeleza kwamba Simba imekwenda Zanzibar kwa ajili ya kunoa makali na itarejea siku moja kabla ya mechi ama siku ya mechi.
     “Vijana wameondoka mchana huu kwenda Zanzibar kwa ajili ya kwenda kusaka makali ya kuwaua Yanga, hivyo nadhani watakaa kule kwa siku tatu au nne na kurejea jijini Dar es Salaam,”Alisema kiongozi mmoja wa Simba. 
    Kwa upande wa Yanga ambayo kwa siku za hivi karibuni imeonekana kutetereka na hatimaye kuutema ubingwa wake,kama mambo yakienda vizuri nayo huenda ikahamisha kambi yake. 
    kiongozi mmoja wa Yanga ambaye hakupenda kutajwa jina lakealisema jana kwamba wanaangalia uwezekano wa kuihamisha timu kutoka Jangwani hadi mahala pengine iwe ndani au nje ya jiji la Dar es Salaam. 
    Mchezo baina ya timu hizo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia iliyonazo timu hizo pindi zinapokutana kwa miaka kadhaa hivi sasa ambapo katika mzunguko wa kwanza, Yanga iliifunga Simba bao 1-0 lililopachikwa na Mzambia Davies Mwape. 
    Wakati Simba inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 59, Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 49.

    SORCE: DINA ISMAIL (mamapipiro.blogspot.com)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MNYAMA AENDA ZENJI KUKUSANYA NGUVU ZA KUCHANA KANDAMBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top