• HABARI MPYA

    Wednesday, April 25, 2012

    YANGA WAITISHA SIMBA, WAIKUNG'UTA ARBA JKT OLJORO


    Yanga SC, mechi inayo na Simba

    YANGA, imekumbuka shuka, wakati kumekucha baada ya jana kuichapa JKT Oljoro mabao 4-1, katikamchezo  Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, mjini Arusha.
    Kwa matokeo hayo, Yanga imeweza kufikisha pointi 49 huku ikiendelea kushika nafasi ya tatu, baada ya Azam kufikisha pointi 50 inayoshika nafasi ya pili, wakati Simba inaongoza kwa pointi  59.
    Yanga ambao walikuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, imelitema kombe hilo, baada kuboronga mechi mbili huku ikinyang'anywa pointi tatu na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania.
    Kamati hiyo, ilichukua uamuzi huo, baada ya Yanga kumchezesha, Nadir Haroub 'Cannavaro' katika mechi yao dhidi ya Coastal Union, iliyochezwa Machi 31, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
    Yanga ilimtumia mchezaji huyu ambaye alikuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekudu kutokana na kumshambulia mwamuzi Israel Nkongo, aliyechezesha mechi yao dhidi ya Azam, Machi 10, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Hata hivyo, matarajio ya Yanga kupata nafasi ya  kuiwakilisha nchi katika michuano ya Afrika mwakani ni finyu, kwani imesaliwa na mechi moja dhidi ya Simba itakayochezwa Mei 5, mwaka huu, Uwanja wa Taifa.
    Katika mechi hiyo, Yanga ikishinda itafikisha pointi 52, ambapo Azam itakuwa na uwezo wa kufikisha pointi 56 iwapo itashinda michezo miwili dhidi ya Toto African na Kagera Sugar, huku ikisubiri hatma ya matokeo ya mechi yao  dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo juzi ulivunjika kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
    Mechi hiyo, ilivunjika  baada ya timu hizo kufunga bao 1-1, lakini mwamuzi wa mchezo huo Rashid Msangi kutoka Dodoma, alivunja pambano hilo, kwa madai Mtibwa waligomea penelti..
    Katika mchezo wa  kwanza uliochezwa kwenye
    Katika mchezo huo wa jana,  Yanga iliandika bao  dakika ya 36 likifungwa na Hamisi Kiiza, kabla ya Haruna Niyonzima kufunga la pili  dakika 40.
    Yanga ikicheza bila Kocha mkuu wake, Kostadin Papic, Kiiza alifunga bao la tatu ikiwa ni dakika moja kabla ya kwenda mapumziko ambapo Pius Kisambale akihitimisha 'sinia' la mabao katika dakika 84.
    Bao la kufutia mafunzo la JKT Oljoro lilifungwa na kwa njia ya penelti.
    Ligi hiyo, inatarajia kuendelea leo kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kwa timu ya Azam itakapoivaana na Toto African.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WAITISHA SIMBA, WAIKUNG'UTA ARBA JKT OLJORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top