• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 26, 2012

  CHEKA AKUBALI DILI LA KUMTWANGA KASEBA


  Cheka kuliaakisaini mbela ya promota Kaike Siraju katikati

  BINGWA wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro  amesaini mkataba wa kupigana na  bingwa wa Kick Boxing. Japhet  Kaseba katika uzito wa Middle utakaofanyika Julai 7, mwaka huu mjini Dar es Salaam
  Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Cheka amesema anashukulu kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mchezo wa masumbwi na mabondia wengi wanamtaka   kupigana  na yeye.
  “Najua mabondia wa hapa bongo kila mtu anataka kucheza na mimi tu wanajua mimi ndio nalipa kwa soko la bongo na nitahakikisha kila anaekuja mbele yangu namtandika kifupi Tanzania akuna bondia mwenye uwezo zaidi yangu,” alisema Cheka.
  “Kaseba nilimpiga kwa KO Oktoba 3, mwaka 2009, anataka tena wembe kwa  ngumi ni sehemu ya maisha yangu, siwezi kukataa na mimi ndio napata riziki yangu humu, hivyo nitahakikisha anayekuja mbele yangu namtwanga tu bila huruma, nitaanza na Mada Maugo Aprili 28 na huyo namuweka kama kiporo
  Naye Promota wa mpambano huo, Kaike Siraju amesema mbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHEKA AKUBALI DILI LA KUMTWANGA KASEBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top