• HABARI MPYA

  Tuesday, April 24, 2012

  MOURINHO AFUNGUKA KUEKELEA MECHI NA BAYERN KESHO


  Football | Champions League


  Jose awania kupendezesha rekodi
  KOCHA Jose Mourinho amepoteza mechi tatu kati ya tano za Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na anatarajiwa kuimarisha rekodi yake wakati atakapoiongoza Real Madrid yake dhidi ya Bayern Munich kwenye mchezo wa marudiano kesho.
  Akiwa Chelsea, Mourinho alitolewa na Liverpool mwaka 2005 na 2007, wakati alipotua Real alitolewa na wapinzani wake Barcelona msimu uliopita, ingawa aliwatuhumu UEFA kuwapendelea wapinzani wake hao.
  Mabingwa mara tisa Ulaya, Real lazima izinduke kwenye kipigo cha 2-1 kwenye mechi ya kwanza na kuitoa Bayern Munich, ili kujikatia tiketi ya kucheza fainali mjini Munich mwezi ujao.
  Real wanaingia kwenye mchezo huo wakitoka kuifunga 2-1  Barca Jumamosi.
  Mourinho, ambaye aligoma kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya mechi za La Liga katika wiki za karibuni, lakini amelazimika kufanya hivyo kabla ya mechi hizi za Ulaya zinazosimamiwa na UEFA, kuzungumzia madudu ya marefa.
  "Sina bahati kiasi hicho kwenye Nusu Fainali," alisema Mourinho katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo. "Nilifungwa moja (dhidi ya t Liverpool) wakati mpira haukuvuka mstari - ambayo ilikuwa ngumu kuamini.
  "Msimu mwingine  (mwaka 2007) nilifungwa kwa penalti - ambayo zaidi ni jamo la bahati mbaya tu - na msimu uliopita (dhidi ya Barca) nilipoteza Nusu Fainali katika njia ambazo kila mmoja anafahamu.
  "Safari natumai kushinda, japokuwa tulifungwa mechi ya kwanza kwa bao ambalo lilikuwa la kuotea," alisema Mourinho ambaye amebeba taji hilo mara mara mbili, akiwa na Porto mwaka 2004 na Inter Milan 2010.
  "Marefa  (kwa ujumla) walikuwa wazuri sana, alifanya kosa, lakini wote tunafanya makosa pia."


  UBORA WA BARCA
  Kiwango kizuri cha Real nyumbani msimu huu, kinafanya wapewe nafasi ya kucheza fainali ya michuano hiyo na mshindi mkati ya Barca na Chelsea.
  Klabu ya London ipo mguu mmoja mbele, kufuatia ushindi wa  1-0 katika mchezo wa kwanza, wakati wenyeji na mabingwa watetezi wanaugulia pia kipigo cha kwanza katika ligi ya kwao kutoka kwa Real ndani ya mechi nane na kuweka rehani taji lao la La Liga.
  Real imeshinda mechi 10 kati ya mechi zao 11 zilizopita kwenye Ligi ya Mabingwa na wametumbukiza nyavuni mabao 22 katika mechi tano walizocheza  Bernabeu kwenye michuano ya mwaka huu.
  Pia wana rekodi ya kuvutia dhidi ya wageni kutoka Ujeruman, wakishinda mechi 17 kati ya  22 na sare tatu.
  Hata moja inayowakabili Real hata wakifuzu kuingia fainali, ni kuwapoteza wachezaji wake wanne - Gonzalo Higuain, Xabi Alonso, Sergio Ramos na Fabio Coentrao -ambao wanaweza kukosa mechi hiyo iwapo watapewa tena kadi za njano na kesho. Mourinho said that was not an issue.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOURINHO AFUNGUKA KUEKELEA MECHI NA BAYERN KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top