• HABARI MPYA

    Wednesday, April 25, 2012

    NANI ALICHEZAJE, ANASTAHILI POINTI NGAPI


    Víctor Valdés
    46
    199
    5.0
    Alikuwa ana uwezo wa kumzuia  Ramires kufunga, lakini alishindwa na kushuhudia nyavu zake zikinesa. Aliokoa mashuti ya mbali ya kipindi cha pili.
    Gerard Piqué
    75
    128
    6.5
    Hatimaye alirejea kikosini Barca na alionekana kupiga mzigo wa uhakika alipokuwa uwanjani, akiondosha mipira kwenye eneo la hatari. Hakuwa mwenye bahati alipogongana na Valdes na kuumia hadi kutoka nje.
    Carles Puyol
    52
    144
    6.5
    Shujaa na anayejituma katika beki kama kawaida yake, lakini alikuwa na machache ya kufanya wakati Chelsea iliposhambulia kwa kasi. Alipeleka kichwa chake kwenye krosi kadhaa hadi mwisho.
    Cesc Fàbregas
    54
    163
    5.5
    Bado yupo chini ya kiwango, lakini alitengeneza nafasi nzuri kwenye lango la wapinzani. Mwishowe mpira haukumkubali sana licha ya juhudi za kusaka mabao, ambazo ziliishia kumfanya asababishe penalti, baada ya kuchezewa rafu na Drogba.
    Xavi
    56
    138
    6.0
    Kiungo mwingine wa Barca ambaye alionekana kucheza chini ya kiwango chake mwishoni, lakini nyota huyo Hispania, alikaza kwenye nafasi ya kiungo na Barca ikafanikiwa kutawala zaidi mpiral. Hata hivyo, hakuwa mwenye madhara sana.
    Andrés Iniesta Luján
    87
    114
    6.0
    Lilikuwa ni bao lake ambalo lilivunja mioyo ya Chelsea mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa na usiku huu alifunga bao safi la pili na kuifanya Barca iongoze 2-0 . Alianzia upande wa kushoto, lakini ilimuwia vigumu kutengeneza nafasi dhidi ya ukuta mgumu wa Chelsea.
    Javier Mascherano
    46
    145
    6.0
    Akiwa amefanya makosa kwenye mechi mbili zilizopita, alionekana mwenye kujiamini katika safu ya walinzi watatu wa Barca. Alijaribu bahati yake kwa mashuti ya mbali kwenye lango la wapinzani wake, lakini hakufanbkiwa kufunga. Ilionekana shuti lake la mwisho likiokolewa na Cech.
    Sergio Busquets Burgos
    60
    138
    6.5
    Barcelona haswa haikuhitaji kiungo mkabaji kwenye mechi hii, kwa sababu Chelsea walihofia kushambulia, lakini Mkatalunya huyo alifanya kazi yake vizuri na alikuwa upande wa kulia katika wakati mwafaka na kuifungia timu yake bao la kuongoza baada ya kazi nzuri ya Cuenca kuipasua ngome.
    Alexis Sánchez
    A46
    163
    5.0
    Alipoteza nafasi mbili za wazi mno katika mechi ya kwanza, lakini hakuwa mwenye bahati usiku huu iliposhuhudiwa kasi yake ikishindwa kuiumiza Chelsea. Zaidi atakumbukwa kwa kumponzsa  John Terry kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
    Lionel Messi
    127
    341
    5.0
    Alionekana kufifia mwishoni mwa mechi na hakukuwa na tofauti katika mchezo wa leot. Alifanya kazi nzuri wakati fulani ya kuwatengenezea nafasi wachezaji wenzake, baadhi kwa kuwawekea mipira kwenye njia, lakini alikosa penalti ambayo ingeipeleka  Barca fainali. Hivyo shujaa huyo usiku huu hakuwa lolote.
    Joan Isaac Cuenca Lopez
    56
    135
    6.0
    Alitengeneza nafasi za kusogeza sogeza, lakini mbonu zake katika wingi  hazikuzaa matunda. ilikuwa ni pasi yake yenye akili ambayo ilimpa Busquets nafasi ya kufunga bao la kuongoza, lakini angeweza kumtungua Cech kwa nafasi nzuri aliyopata kipindi cha pili.
    • Waliotokea benchi
    Daniel Alves
    44
    131
    5.0
    Ajabu aliachwa kwenye kikosi cha kwanza cha Guardiola, ambacho kilianza na mabeki watatu na hakuonekana kama kawaida yake hata alipoingia kuchukua nafasi ya  Pique. Hakuwa tayari kuiumiza Chelsea na krosi zake zilikuwa mbovu.
    Seydou Keita
    31
    127
    5.0
    Aliingia kipindi cha pili, lakini alikuwa na faida chache.
    Tello
    32
    131
    5.0
    Aliachwa nje leo baada ya kiwango kibovu alichoonyesha kwenye Clasico na hakufanya makubwa sana alipoingia uwanjani. Alipoteza nafasi moja nzuri mwishoni mwa mchezo.
    Petr Cech
    Nyota wa mchezo
    491
    8
    7.5
    Alikuwa shujaa wa timu yake kwa kuokoa michomo mingi ya hatari, zaidi ya kukumbukwa ni Cuenca, Mascherano na Messi. Asingeweza kufanya chochote kwa mabao aliyofungwa na alikuwa mwenye furaha kuona mkwaju wa penalti unagonga mwamba.
    Branislav Ivanovic
    229
    55
    5.5
    Alikuwa shujaa wa safu ya ulinzi kwa uchezaji wake wa nidhamu, alikuwa akifika maeneo yote. Alizima jitihada za  Alexis na badaaye Tello, lakini mabao yote yalipitia kwenye eneo lake.
    Ashley Cole
    287
    13
    7.0
    Alionyesha kiwango cha hali ya juu mno katika beki ya pembeni, ambaye alimuweka Cuenca katika ulinzi mkali na hakuwapa furaha wapinzani wao kwenye upande wake wa Uwanja. Alilinda vizuri.
    Gary Cahill
    205
    22
    6.0
    Alikuwa ana mwanzo mbaya katika mchezo huo na ilikuwa atolewe, lakini alifanya vizuri baadaye uwaniani.
    John Terry
    Aliyetokoa zaidi
    160
    231
    3.5
    Alifanya kazi nzuri kwa ukabaji wake wa makini na nguvu, lakini alijishushia heshima alipompiga kiatu Alexis kwa nyuma na alistahili kadi nyekundu. Alionekana dhahiri kuigharimu timu yake kukosa nafasi ya kusonga mbele. Achana na hayo, lakini atakosa fainali.
    Ramires
    381
    9
    7.0
    Lilikuwa ni bao lake liliwarudishia matumaini Chelsea wakati Barca walikuwa mbele na wenye kujiamini. Alifanya jitijada nzuri, lakini Valdes angeweza kuokoa. Alijituma sana na alkikuwa mchango mkubwa.
    Frank Lampard
    274
    20
    6.0
    Hakuthubutu kusita kupigana uwanjani jambo ambalo lilikuwa muhimu kwa timu yake, alitumia uzoefu wake wote na alitumia nafasi chache alizopata kufanya mambo adimu. Aliitumia mipira vizuri alipokuwa nayo, lakini alichezea kwenye ulinzi zaidi. Alipewa kadi ya njano.
    John Obi Mikel
    192
    56
    5.0
    Alizuia vizuri kiasi fulani, lakini alikuwa akipoteza mipira na angepewa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Alexis.
    Raúl Meireles
    213
    30
    6.0
    Alifanya vema katika ulinzi, na aliwakatalia wachezaji wa kiungo wa Barca kutawala mpira. Alitumia muda mwingi katika kujilinda lakini alishindwa kupeleka mipira mingi mbele. Alipewa kadi ya njano mwishoni.
    Juan Mata
    159
    70
    5.0
    Kwa mara nyingine alikuwa si kitu. Alicheza ovyo London na hakuvutia hapa pia. Alishindwa kuzinduka mchezoni pamoja na kwamba mbonu na timu yake hazikusaidia. Alitolewa dakika za lala salama.
    Didier Drogba
    264
    58
    5.5
    Ni mwenye bahati mno kuepuka lawama za leo, baada ya kumuangusha Cesc na kusababisha penalti. Alionekana kidogo mbele ya mpira, lakini bao lake katyika mechi ya kwanza limechangia ushindi huu. Alimpisha  Torres mwishoni.
    • Waliotokea benchi
    José Bosingwa
    217
    18
    6.5
    Aliingia kuchukua nafasi ya majeruhi Cahill na alionyesha kiwango kizuri wakati Chelsea ikijilinda.
    Fernando Torres
    469
    23
    7.0
    Labda hakuwa na msimu mzuri huu, lakini kuingia na kwenda kufunga bao la dakika za lala salama, ambalo lilivunja mioyo ya  Barcana kuihakimkishia  Chelsea kucheza fainali, ilikuwa babu kubwa.
    Salomon Kalou
    184
    37
    5.0
    Aliingia kuchukua nafasi ya Mata kipindi cha pili na alifanya kazi nzuri kidogo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NANI ALICHEZAJE, ANASTAHILI POINTI NGAPI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top