• HABARI MPYA

  Wednesday, April 25, 2012

  RONALDO: KUWAFUNGA BAYERN KAMA KUMSUKUMA MLEVI


  Cristiano Ronaldo - Real Madrid
  Cristiano Ronaldo - Real Madrid
  MSHAMBULIAJI wa Real MadridCristiano Ronaldo anaamini kwamba timu yake itaifunga Bayern Munich leo katika nusu Fainali ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Santiago Bernabeu.

  Klabu hiyo ya Jiji la Hispania, lazima ikipiku kichapo cha mabao 2-1 kwenye Uwanja wake ili kutinga fainali itakayopigwa mjini Munich, Mei 19. Na nyota wake huyo anaamini mechi na vigogo hao wa Ujerumani itakuwa ngumu, lakini hana shaka kwamba Madrid itaibuka mshindi.

  "Tunajua kwamba Bayern watashambulia kwa kushitukiza , lakini pia tunafikiri kwamba watatuheshimu kwa kiasi kikubwa kwa sababu tutacheza nyumbani,"alisema akihojiwa na bwin.com.

  "Tuko vizuri na nina uhakika kwamba tutashinda nyumbani kwa sababu tutacheza katika Uwanja wetu, mbele ya mashabiki wetu tuna mazingira yote ya kuwa tayari kushinda."

  Alipoulizwa kuhusu ubora wa Bayern, Mreno huyo aliwaonya wachezaji wenzake kuwa makini na safu ya ushambuliaji ya Bavarian, kwani ni tishio.

  "Mario Gomez, ambaye ni mshambuliaji na mmoja wa wafungaji bora katika Ligi ya Mabingwa, Franck Ribery na Arjen Robben wite ni hatari sana," alisema. "Tutatakiwa kuwa makini sana kwa watu hao wanne ambao wanacheza mbele, kwa sababu mmojawao atajaribu kuleta tofauti."

  Msimu wa tatu kwa Ronaldo Madrid unaelekea ukingoni na kijana huyo mwenye umri wa miaka  27 amehakikisha hafikirii kwenda popote.

  "Mwaka baada ya mwaka, najaribu kuonyesha ubora wangu nikiwa na jezi hii," alisema. "Mambo yanakwenda vizuri upande wangu na ninataka kuendelea hivi."
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO: KUWAFUNGA BAYERN KAMA KUMSUKUMA MLEVI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top