• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 25, 2012

  JT AOMBA RADHI, AKUOMBA RADHI HADI WEWE MPENZI CHELSEA


  UEFA Champions League : John Terry - Cuneyt Cakir, FC Barcelona v FC Chelsea
  Terry akilimwa nyekundu
  NAHODHA wa ChelseaJohn Terry ameomba radhi kwa kadi nyekundu alitopewa katika sare ya 2-2 dhidi ya Barcelona, lakini amesema kutolewa kwake haziwazuia kusherehekea tiketi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

  Nahodha huyo Chelsea alilimwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 37 baada ya kumkwatua Alexis Sanchez kwa nyuma, na sasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31-atakosa fainali itakayopigwa mjini Munich mwezi ujao.

  "Sanchez alikuwa anazingua nyuma yangu wakati huo. nimeona marudio na inaonekana ni mbaya, lakini mimi sina ya mchezaji wa kudhamiria kumfanyia baya mtu yeyote," alisema Terry. "Niliinua mguu wangu ambao labda sikupaswa kuupeleka eneo hilo. Natumai, watu wa huko ambao wananijua mimi vizuri kama mchezaji na mtu ambaye siko hivyo.

  "Nilihisi nimewaangusha wachezaji wenzangu na nimewaomba radhi na ninataka kuomba radhi kwa mashabiki wa Chelsea nao pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JT AOMBA RADHI, AKUOMBA RADHI HADI WEWE MPENZI CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top