• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 25, 2012

  PEP ASEMA YOTE YA MOYONI, HADI CHOZI, UTAMHURUMIA


  Pep Guardiola - Barcelona
  Pep Guardiola - Barcelona
  KOCHA wa BarcelonaPep Guardiola amekubali matokeo ya sare ya 2-2 jana na Chelsea kwenye Uwanja wa nyumbani Camp Nou na amesema haoni ambako vijana wake walikosea, ingawa alibubujikwa machozi kwa uchungu.

  Wakalunya hao wametolewa Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya The Blues kushinda mechi ya kwanza 1-0 Uwanja wa Stamford Bridge.

  Barca ilionekana kutanguliza mguu mmoja fainali, baada ya mabao ya Sergio Busquets na Andres Iniesta kuwapa vigogo hao wa Hispania uongozi wa mechi 2-0, lakini Ramires na Fernando Torres waliisawazishia The Blues.

  Guardiola alisema asingeweza kuwaambia wachezaji wake wacheze kwa kujihami na akasikitikia timu yake kutokuwa na bahati mbele ya lango la wapinzani.

  "Tulifanya kila tulichoweza, lakini tumefeli," alisema baada ya mechi hiyo. "Hatukupata bao katika wakati muhimu, na hivyo vitu vinagharimu. Sasa, lazima tuzinduke na tufikirie msimu ujao. Kitu pekee tunachoweza kufanya ni kuwapongeza Chelsea kwa kazi yao nzuri ya kulinda lango lao.

  "Niliwaambia wachezaji wangu washambulie bila kusita, kwa sababu hilo ndilo tulitakiwa kufanya. Na kisha bao la kwanza Chelsea lilipokuja. Lakini tulikuwa tuna uhakika bado, tumekuwa hivi wakati wote. nitajifunza kutokana na hili. sitaki kuhisi. nawaangalia wachezaji wangu na sijui nini cha kuwaambia walikosea wapi, kwa sababu sijaona kosa lolote walilofanya."

  Kocha huyo wa Kispanyola amesema hana hasira na Lionel Messi, ambaye alipoteza nafasi ya kufanya Barca iongoze 3-1 mapema kipindi cha pili, alipokosa penalti.

  "Naweza kumshukuru kwa yote aliyofanya,"alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 41. "Jinsi ninavyomzikia yeye ni hakuna mfano, ametusaidai kuimarika kila siku. Atakuwa na saa kadhaa ngumu, kwa sababu sote tunajua ni mshindani kiasi gani, lakini hilo ni jambo zuri juu ya mchezo huu. Wakati mwingine anatabasamu, na wakati mwingine unafungwa."
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PEP ASEMA YOTE YA MOYONI, HADI CHOZI, UTAMHURUMIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top