• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 27, 2012

  AZAM: HATUTANII, TUNATAKA UBINGWA


  Wachezaji wa Azam, Said Mourad na John 'Mabao' Bocco 'Adebayor'

  OFISA wa Azam FC, Patrick Kahemele ameandika kwenye ukurasa wake Facebook kuelezea nia ya klabu hiyo kuutaka ubingwa wa Ligi Kuu, wanaogombea kwa pamoja na Simba SC.
  SOMA:
  “Tatizo timu za Tanzania kama walivyo mashabiki wake ni Simba & Yanga, wachezaji, makocha, viongozi hadi mashabiki wao wamekalia uwakala wa kuzisaidia Simba na Yanga. Kama Azam FC ingekuwa inashika nafasi ya saba (7) ikiwa pointi 15 nyuma ya Simba na Yanga msingesikia refa kupigwa wala nini lakini kwa kuwa kwenye mechi za Azam FC zinaamua nafasi ya Simba/Yanga kwenye ubingwa na uwakilishi wa nchi kimataifa basi unashangaa watu wanakuja kuhakikisha wanaisimamisha Azam FC ili wawafurahishe Simba au Yanga.... Tanzania ni nchi ambayo viongozi wa vilabu vya ligi kuu ni wanachama wa Simba/Yanga tena wanahudhuria mikutano na kupiga kura, ...... hawa watu wanakuja viwanjani na chuki, jazba na unazi. Tanzania ni nchi ambayo timu zipo tayari kushuka hata daraja lakini wawe wametimiza azma yao ya kuzisaidia Simba/Yanga. ni kipindi cha mpito na kitapita, ndiyo maana tunapigania mpira wetu uwe kwenye TV ili mambo yanayofanyika kila mtu aone. Azam FC haikatishwi tamaa na itaendelea kupambana na dhamira yetu ni kuhakikisha tunaleta kikombe cha Afrika in the next five years.
  Waliwatisha na baadaye kuwashusha daraja baadhi ya timu ambazo zilikuwa zinaleta Challenge, wamejaribu kwa Azam FC wameshindwa na hakika hawataweza kamwe. Hii ni nchi ambayo mashabiki wake walishangilia Moro United ya Balhabou kuukosa ubingwa wakati ilikuwa ikiongoza kwa pointi 13 huku ligi ikiwa imebakiza mechi 5 tuu.... leo walitaka Azam FC ifungwe mfululizo ili Simba na Yanga zipate nafasi, Tunasema tutapambana hadi mwisho wa ligi... na Ubingwa Tunautaka,”AMEMALIZA.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM: HATUTANII, TUNATAKA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top