• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 30, 2012

  TUNAHITAJI UKUMBI BORA WA NDONDI


  Mchezo wa ngumi katika nchi yetu ya Tanzania unazidi kushika kasi
  kutokana na kuchipuka kwa mabondia wengina mapromota ambao wanapigana
  katika kuwania mataji mbalimbali nje na ndani ya Tanzania na kuandaa
  mapambano . wapo mabondia wengi katika historia ya Tanzania ambao
  wamewahi kupigana nje ya nchi hukiwauliza kuhusu ubora wa mchezo wa
  ngumi katika upande wa vifaa vya mchezo huo ndani ya nchi yetu ni
  imani yangu waliowengi wanaweza kukubaliana nami kuwa bado unahitaji
  vitu muhimu ili kuendeleza mchezo huo .
  
  Kwa Tanzania tumekuwa na mabondia wengi ambao wameweza kutingisha nje
  ya Tanzania kama Joseph Marwa, Rashid Matumla, Rogers mtagwa Ally Kimweri na
  Emanuel Mrundwa ambao waliweza kutwaa mataji mbalimbali ya mchezo huo
  . jambo moja kuu ambalo watanzania tunalisahau ni kukosekana kwa kumbi
  bora ya mchezo huo kwa upande mwingine kuna wakati baadhi ya watu
  wanaohusika na mchezo wa ngumi waliwahi kuwa na wazo hilo lakini
  nimeona jumatatu ya leo nijaribu kulitilia mkazo .natoa mfano kama
  tulivyo weza kujenga uwanja wa taifa na kuziona nchi kubwa duniani
  zikija kucheza mechi za kirafiki kama Brazil basi hata mchezo wa ngumi
  linawezekana ukitazama kama marekani ambao mchezo huu umekuwa kwa
  kiwango cha juu kutokana nchi hiyo kuboresha maeneo ya kuchezea
  kumbuka silinganishi kiwango cha mchezo bali ni namna ya kuboresha.
  
  Kwa Tanzania vipo vyama vingi vya mchezo wa ngumi PST,TPBC,TPBO bila
  kusahau kile cha taifa cha BFT lakini ni mara kadhaa Makore Mashaga
  katibu mkuu wa BFT amekuwa akizungumzia juu ya ukosefu wa vifaa maeneo
  ya mazoezi na kumbi za kupigania vimekuwa ni vikwazo vikubwa kwa
  mchezo huo kwa Tanzania kwakuwa serikali imeweza kuleta uwanja mpya wa
  mpira wa miguu ambao hata Suleiman nyambui anafaidika nao alikadharika
  wanamuziki kupata studio ya kisasa ya kurekodia muziki bila shaka
  mchezo wa ngumi nao unahitaji eneo zuri la kuchezea mchezo huo kama
  ilivyo Las Vegas Nevada na MGM Grand au Madson square ni dhahiri
  inawezakana kwa Tanzania kuwa na kumbi bora ya kisasa na imani vyama
  vya mchezo wa ngumi vyote nchini vinaweza kukaa chini na kujadiliana
  na serikali kupitia wizara ya habari utamaduni na michezo kuhakikisha
  tunapata kumbi bora ya kisasa ya kupigania ili kuongezea ujuzi na
  viwango vya mchezo wa ngumi kwa Tanzania.
  
  kama ufilipino imeweza kutoa bingwa wa dunia hata Tanzania inaweza pia
  kwani ukiacha soka mchezo wa ngumi ndio mchezo pekee ambao unakuja kwa
  kasi pengine liwe ombi rasmi kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa
  Tanzania ambaye mwaka jana alitunikiwa tuzo ya heshima ya mwanamichezo
  na chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania TASWA kuwa
  kiongozi bora kwa kujari michezo si vibaya Mh Jakaya Kikwete
  akatuachia wapenzi wa masumbwi kumbi bora w hata mabondia wanje
  wajekupambana Tanzania kama zinavyokuja timu kubwa za mpira dunia
  kucheza uwanja wa taifa .
  
  nina maliza kwa kusema kuwa ni imani yangu kuwa kwa kujengwa uwanja
  huo kutawapa mabondia wa tanzania kujiaamini na kuupanua mchezo huo
  na unaweza pia kulitangaza jina la Tanzania katika Nyanja za utalii
  ndani na nje ya Tanzania kama inavyowezekana kuleta mastaa wa wakubwa
  wa muziki kutoka ulaya na amerika ni dhahiri hakuna lisilowekana kwa
  Tanzania .
  
  -- 
  Super D Boxing Coach
  Email.superdboxingcoach@gmail.com
  www.burudan.blogspot.com
  www.superdboxingcoach.blogspot.com
  Mob;+255787 406938
  +255774406938
  Po.Box. 15493
  Dar es Salaam Tanzania
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TUNAHITAJI UKUMBI BORA WA NDONDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top