• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 24, 2012

  TALIB HILAL KOCHA MPYA AL AHLY


  Talib Hilal

  BEKI wa zamani wa kati Simba SC, Talib Hilal ameteuliwa kuwa kocha wa klabu ya Al Ahli ya Dubai ya soka ya ufukweni, ambayo itashiriki michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia.
  Akizungumza na bongostaz.blogspot.com jioni hii kutoka Oman anakoishi, Talib aliyewahi pia kuwa kocha wa muda wa Simba zaidi ya mara mbili, alisema anatakiwa kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya mashindano hayo, yaitwayo MONDIALITO 2012 yatakayofanyika Jijini Sao Paulo, Brazil kuanzia Mei 16 hadi 22.
  Talib aliyewahi kuwa pia kocha wa timu ya taifa ya vijana ya Oman na kocha Msaidizi wa timu ya wakubwa ya nchi hiyo, anakumbukwa zaidi Simba kwa mchango wake ulioiwezesha klabu hiyo kuitoa Zamalek mwaka 2003 katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TALIB HILAL KOCHA MPYA AL AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top