• HABARI MPYA

  Thursday, April 26, 2012

  GUARDIOLA ABWAGA MANYANGA BARCA, BIELSA KOCHA MPYA CAMP NOU


  bielsa-guardiola
  Bielsa kulia na Guardiola
  KOCHA Pep Guardiola atapenda kuachia ngazi Barcelona mwishoni mwa msimu na klabu hiyo tayari imemtambulisha Marcelo Bielsa kama mrithi wake, bongostaz.blogspot.com imeipata hiyo kutoka Goal.com usiku huu.

  Mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa wa Hispania alikutana na rais wa Blaugrana, Sandro Rosell na Mkurugenzi wa Michezo, Andoni Zubizarreta leo na kuwaeleza nia yake ya kuachia ngazi baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitatu.

  Guardiola, ambaye ameiongoza Barca kutwaa mataji 13 tangu aanze kazi, atathibitisha nia yake ya kuacha kazi kwa wachezaji wake kesho asubuhi atakapokutana nao na inaaminika baada ya hapo atatoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari katika mkutano uliopangwa kufanyika saa 5:00 asubuhi kwa saa za huko.

  Klabu hiyo inapanga kumchukua kocha wa Athletic, Bielsa atue Camp Nou. Muargentina huyo anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu na anakubalika mno mbele ya bodi ya wakuruigenzi ya Blaugrana, kama ambavyo Guardiola, amemtaja Bielsa kuwa kocha bora katika soka ya leo. Inaaminika, Guardiola pia aliulizwa kuhusu Bielsa kuchukuliwa Catalunya.

  Kama kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 ataamua kubaki Uwanja wa San Mames, Barcelona itahamishia ndoana zake kwa mmojawapo katika ya makocha wanaokubalika kwa Guardiola, hao ni Msaidizi wake Tito Vilanova, kocha wa zamani wa timu B, Luis Enrique, ambaye kwa sasa anaifundisha Roma, au kocha wa zamani wa timu ya vijanaOscar Garcia.

  Ikikwama huko, Barca itamgeukia kocha wa zamani wa Villarreal, Ernesto Valverde au makocha wa kigeni kama kutoka Mjerumani Joachim Low, lakini Wakurugenzi wa klabu hiyo watafanya yote hayo baada ya kujiridhisha wamemkosa kabisa chaguo lao la kwanza, Bielsa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  1 comments:

  Anonymous said... April 28, 2012 at 10:40 AM

  bielsa z the best coach by this time because the pressure for success at bilbao z not highly to that of catalans guys bt he can make it though it will tough for him due to the pressure exists now at camp nou following exit in Champions league and La Liga position to take the trophy being to Mourinho's side...........

  Item Reviewed: GUARDIOLA ABWAGA MANYANGA BARCA, BIELSA KOCHA MPYA CAMP NOU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top