• HABARI MPYA

  Friday, April 27, 2012

  MINZIRO: MNYAMA ATAKUFA, NA OLE WENU YANGA VISOKOROKWINYO


  Minziro kulia akiwanoa wachezaji wa Yanga


  KOCHA Msaidizi wa timu ya soka ya Yanga, Fred Minziro (pichani kushoto) amesema ushindi mnono wa mabao 4-1 iliyoupata timu yake juzi dhidi ya JKT Oljoro ni maandalizi tosha kwa ajili ya pambano lao na Simba.
  Minziro alisema wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wako tayari kwa pambano hilo na kwamba Simba isitarajie mteremko katika mchezo huo hata kama Yanga imekosa nafasi mbili za juu.
  ‘’Naenda kupambana na Simba kulinda heshima yangu binafsi na ya Wanayanga, hivyo Simba wasitarajie kupata ubingwa wao kwa kutufunga hilo halitakubalika kamwe, ‘’alisema.
  Aliwaomba mashabiki wa Yanga watulie na kwamba kushindwa kutwaa ubingwa mwaka huu itakuwa kichocheo cha kutwaa ubingwa msimu ujao.
  Alisema kuanza kuoneshana vidole kwa nini Yanga imepoteza ubingwa si jambo mwafaka na kwamba kinachotakiwa ni viongozi wa Yanga kusubiri taarifa ya benchi la ufundi ili waweze kuifanyia kazi.
  ‘’Hakuna mwana-Yanga mwenye uchungu na timu halafu adiriki kuihujumu na kama kuna mtu wa namna hiyo huyo hafai na hawezi kuwa Yanga wa kweli kwani anaweza kuwa mamluki,’’ alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MINZIRO: MNYAMA ATAKUFA, NA OLE WENU YANGA VISOKOROKWINYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top