Mshambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba akishangilia bao lake pekee alilofunga dakika ya pili ya dakika za majeruhi baada ya kutimu dakika 45 za kipindi cha kwanza kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, London, England usiku huu katika Nusu Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, dhidi ya mabingwa watetezi, Barcelona ya Hispania. Chelsea sasa inahitaji sare yoyote kwenye mchezo wa marudiano ugenini, Uwanja wa Camop Nou ili kutinga fainali, ambako itacheza na mshindi kati ya Bayern Munich ya Ujerumani na Real Madrid ya Hispania. Mechi ya kwanza jana mjini Munich, Real walifungwa 2-1 na wanahitaji ushindi japo wa 1-0 nyumbani, Santiago Bernabeu ili kutinga Fainali.
MUHIMU KUJUA HAYA...
•The Blues wameendeleza rekodi nzuri ya nyumbani msimu huu
katika Ligi ya Mabingwa, leo wakishinda mechi ya saba katika mechi saba
walizocheza, wamefunga mabao 17 na wamefungwa mawili tu.
•Leo ni mara ya saba kwa timu hiyo ya London kucheza Nusu
Fainali ya Ligi ya Mabingwa ndani ya miaka tisa.
Lakini wameshinda mechi moja tu, walipoifunga kwa jumla ya
mabao 4-3 mwaka 2008. Je, wataitoa Barca Camp Nou?
•Timu hiyo ya Stamford Bridge haijawahi kutwaa Kombe lolote
la Ulaya, zaidi ya kushika nafasi ya pili mwaka 2008.
•Barcelona ilipokwenda mara ya mwisho London, Mei mwaka jana
kwenye Uwanja wa Wembley, iliifunga Manchester United mabao 3-1 na kutwaa taji
la nne la Ligi ya Mabingwa.
•Kama mabingwa hao watetezi watatwaa taji hilo msimu huu,
itakuwa mara ya nne ndani ya miaka saba na itakuwa timu ya kwanza kutetea taji
tangu AC Milan mwaka 1990.
•Kabla ya leo, timu ya mwisho kuifunga Barca katika michuano
hii, ilikuwa ni Inter Milan chini ya Jose Mourinho ambaye sasa anaikochi Real
Madird mwaka 2010.
•Leo Lionel Messi ametimiza
mechi saba anakutana na Chelsea katika Ligi ya
Mabingwa bila kutikisa nyavu za The Blues.
•Wakati timu hizo zilipokutana katika Robo Fainali mwaka
2000, Barcelona iliifunga Chelsea 5-1 katika mechi ya marudiano Uwanja wa Camp
Nou.
Katika mechi hiyo, Roberto Di Matteo alicheza kwenye kikosi
cha kwanza cha The Blues, wakati Pep Guardiola alichezea Barca- leo wote
wanakaa kwenye mabenchi ya timu zao.
•Kabla ya leo, Chelsea ilikutana mara ya mwisho na Barcelona
Mei mwaka 2009, kwenye michuano kama hii na hatua kama hii. Baada ya sare ya
bila kufungana kwenye mechi ya kwanza,
Barca walifuzu kuingia fainali kwa bao la dakika ya mwisho la Andres Iniesta,
ambalo lilikuwa la kusawazisha baada ya Michael Essien kutangulia kufunga. Barca
ilifuzu kwa faida ya bao la ugenini.
VIKOSI VILIVYOCHEZA LEO:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Mikel, Lampard, Meireles, Ramires/Bosingwa dk88, Mata/ Kalou dk 74 na Drogba.
Wa akiba ambao hawakutumika:
Turnbull, Essien, Torres, Malouda, Sturridge
WALIOPEWA KADI ZA NJANO:
Cheldes: Ramires, Drogba
MFUNGAJI WA BAO: Drogba dakika ya 45
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Puyol, Mascherano, Adriano, Busquets, Iniesta, Xavi/Cuenca dk86, Messi, Sanchez/Pedro dk66 na Fabregas/Thiago dk78. Subs WA AKIBA AMBAO HAWAKUTUMIKA:
Pinto, Pique, Bartra, Keita
WALIOPEWA KADI ZA NJANO:
Pedro, Busquets.
MAHUDHURI: 38,039
REFA: Felix Brych (Ujerumani).
0 comments:
Post a Comment