• HABARI MPYA

    Thursday, April 19, 2012

    KIUNGO YANGA ABEBA JIKO LA NGUVU, APANIA KUWAFUNGA SIMBA AMZAWADIE BAO MKEWE

    Aliyewahi kuwa kiungo wa klabu ya Yanga, Ally Msigwa akiwa na mkewe, Tijara Kupaza baada ya kufunga pingu za maisha Machi 30, mwaka huu huko Tanita, Kibaha mkoani Pwani. Mchezaji huyu aliyeibuliwa kutoka timu ya vijana na Profesa Dusan Savo Kondic aliachwa kwenye klabu hiyo wakati akiwa majeruhi. Kwa sasa anachezea Moro United na kwa soka yake kuna wakati aliwahi kutakiwa na Vancouver Whitecaps ya Marekani, lakini majeruhi yalimpotezea nafasi hiyo. Msigwa amesema atawafunga Simba Jumatatu ili kutoa zawadi kwa mkewe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIUNGO YANGA ABEBA JIKO LA NGUVU, APANIA KUWAFUNGA SIMBA AMZAWADIE BAO MKEWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top