• HABARI MPYA

    Saturday, April 21, 2012

    DI MATTEO AMBAKISHA DROGA CHELSEA

    Drogba
    KOCHA Roberto Di Matteo amesema  Didier Drogba ana uwezo wa kubaki Chelsea baada ya msimu huu.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu na baada ya hapo imeelezwa atakubali ofa ya kujiunga na Shanghai Shenhua ya China January.
    Di Matteo alisema anatarajiwa klabu hiyo itamhitaji tena mshambuliaji huyo.
    “Kiwango cha Didier uimara wake vinamfanya astahili kuendelea kucheza Ligi Kuu akiwa Chelsea, au nyingine yoyote mwakani,” alisema Di Matteo kuwaambia Waandishi katika taarifa iliyotufikia bongopstaz.blogspot.com.
    "Anaweza kuendelaea kucheza kwa miaka kadhaa katika kiwango hiki. Hatastaafu."
    Di Matteo bado hana uhakika kama mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ivory Coast atabakia Stamford Bridge katika kipindi chake kilichobaki kwenye soka, lakini anahisi mchezaji huyo tayari ni sehemu ya historia ya klabu hiyo.
    "Iwe niwe popota, sijui," Di Matteo alisema. "Ni sehemu ya historia ya klabu, kama wachezaji wengi, na wakati wote itakuwa hivyo. Lakini uamuzi wa klabu,"alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DI MATTEO AMBAKISHA DROGA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top