BAHATI mbaya iliyoje Chelsea inawasili Emirates ikiwa na lundo
la majeruhi, kuliko wenyeji wao.
The Gunners wamempoteza Mikel Arteta kwa mechi zote
zilizobaki za msimu kwa maumivu ya kifundo cha mguu na anaungana na majeruhi wa
muda mrefu Per Mertesacker, Jack Wilshere vifundo vya mguu kama yeye na
Emmanuel Frimpong goti. Kuna habari njema kuhusu Francis Coquelin na Abou Diaby ambao wote wanatarajiwa kucheza mechi hiyo ya wapinzani wa Jiji la London, lakini Yossi Benayoun hataruhusiwa kucheza kwa mujibu wa mkataba wake mkopo kutoka The Blues.
Chelsea itamkosa Branislav Ivanovic ambaye atakuwa anamalizia adhabu yake ya kusimamishwa mechi tatu baada ya mechi hii.
Katika majeruhi, David Luiz anatarajiwa kukosa wiki nyingine kutokana na maumivu ya nyama za paja aliyoyapata kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA wakiifunga Tottenham.
Ryan Bertrand ni majeruhi wakati Oriel Romeu anaumwa na wote hawatakuwapo leo.
JE WAJUA?
•Arsenal imeshinda mechi 12, sare mbili na kufungwa mechi
mbili katika mechi zao 16 zilizopita Emirates.
•The Gunners watamkosa Mikel Arteta kwa sehemu iliyobaki ya
msimu na hawajashinda mechi ya Ligi Kuu bila ya yeye msimu huu.
•Robin van Persie amefunga mabao 17 katika mechi 19 za klabu
hiyo msimu huu.
•Mshambuliaji huyo wa
Kiholanzi, alipiga hat trick katika ushindi wa 5-3 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja
wa Stamford Bridge, ambako Arsenal iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza tangu
Liverpool mwaka 1996 kutikisa nyavu za Chelsea mara tano.
•Chelsea imeshinda mechi tatu tu kati ya 19 zilizopita ikiwa
mgeni wa Arsenal, lakini zote zinakuwa ni ndani ya mechi sita za mwishoni mwa
msimu.
•The Blues wamefungwa mabao mengi zaidi (18) katika dakika 15
za mwisho zaidi ya klabu nyingine yoyote kwenye Ligi Kuu.
•Didier Drogba amefunga mabao manane katika Ligi Kuu dhidi
ya The Gunners.
•Chelsea imefunga na kufungwa asilimia 95 ya mabao yao ndani
ya boksi – ambayo ni kiwango kikubwa katika ligi.
VIKOSI VYA LEO:
ARSENAL: Szczesny, Sagna, Koscielny, Vermaelen, Santos, Ramsey,
Song, Rosicky, Walcott, Van Persie na Gervinho.
CHELSEA: Cech, Bosingwa, Cahill, Terry, Cole, Lampard,
Essien, Ramires, Mata, Sturridge na Torres.
0 comments:
Post a Comment