• HABARI MPYA

  Sunday, June 04, 2023

  YANGA YAICHAPA USM ALGER 1-0, YAKOSA KOMBE LA SHIRIKISHO

  WENYEJI, USM Alger wamefanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kufungwa 1-0 na Yanga katika mchezo wa marudiano wa Fainali usiku huu Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria.
  USM Alger wamenufaika na ushindi wa ugenini wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza, kwani pamoja na sare ya jumla ya 2-2, lakini wamefaidika na mabao ya ugenini.
  Katika mchezo wa leo bao pekee la Yanga limefungwa na beki wa kulia, Juma Shabani kwa penalti dakika ya saba baada ya Mkongo mwenzake, Fiston Kalala Mayele kuangushwa kwenye boksi.
  Kipa wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra aliinusuru Yanga kuruhusu bao leo baada ya kupangua mkwaju wa penalti wa beki Zinéddine Belaïd dakika ya 59.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAICHAPA USM ALGER 1-0, YAKOSA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top