• HABARI MPYA

  Monday, June 05, 2023

  RAIS SAMIA AWATAKA YANGA WAMALIZE MZOZO NA FEI TOTO


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ameitaka klabu ya Yanga kumaliza mgogoro wake na kiungo Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ na kwamba hafurahishwi na mizozo ya klabu na wachezaji.
  Akizungumza Ikulu Jijini Dar es Salaam leo wakati wa hafla maalum ya kuwapongeza Yanga kwa kufika Fainali Kombe la Shirikisho Afrika Rais Samia amesema wakitatua mzozo huo wampe mrejesho.
  “Sifurahii kusikia mnakuwa na mizozo na wachezaji, na sitaki kusema mengi, nataka niwaambie tu hii ishu ya Fei Toto hebu kaimalizeni. Kaimalizeni ili tuangalie mbele sasa. 
  Haipendezi klabu kubwa nzuri kama hii iliyofanya kazi nzuri mnakuwa na mizozo na kaugomvi na katoto. Hebu kamalizeni muende vizuri, nitasubiri kupata mrejesho wa hili, siku yoyote mkia tayari karibuni nyumbani mje kunipa mrejesho,” amesema Rais Samia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAIS SAMIA AWATAKA YANGA WAMALIZE MZOZO NA FEI TOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top