• HABARI MPYA

    Tuesday, March 24, 2020

    NDAYIRAGIJE ASEMA ATALAZIMIKA KUUNDA UPYA KIKOSI CHA TAIFA STARS RATIBA MPYA IKITOKA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Etienne Ndayiragije amesema atalazimika kuita wachezaji wapya wa kuunda kikosi cha Taifa Stars mara ratiba mpya itakapotolewa kulingana na uwezo wa wachezaji kwa wakati huo baada ya kuvunja kambi hivi karibuni.
    Taifa Stars ilivunja kambi yake ya kujiandaa na mechi ya kufuzu (AFCON) dhidi ya Tunisia pia kujiwinda na michuano ya Ubingwa wa Mataifa Afrika, (CHAN) inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchin mwao pekee kutokana na kuahirishwa kwa michuano yote sababu ya mlipuko ya virusi vya corona duniani kote.
    Katkati ya mwezi huu, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilisimamisha mechi zote za kufuzu za mashindano ya Afrika kwa ushauri wa Shirika la Afya Dunani (WHO) kwa ugonjwa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona.
    Mechi zilizofutwa ni za tatu za na za nne kufuzu Fainali za AFCON 2021 ambazo zilipangwa kufanyika kati ya Machi 25 na 31 mwaka huu, kufuzu Fainali za Kombe la Dunia la Wanawake chini ya umri wa miaka 20 zilizopangwa kufanyika kati ya Machi 20 na 22 na marudiano Machi 27 na 29 mwaka huu.
    Aidha, CAF pia imesitisha mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa (AFCON) kwa Wanawake 2020 zilizopangwa kufanyika kati ya Aprili 8 na 14 mwaka 2020 – na ratiba mpya ya michuano hiyo itatangazwa kwa wakati.
    Taifa Stars ilikuwa tayari kambini kwa takriban wiki nzima kujiandaa na mchezo wa Kundi J kufuzu AFCON dhidi ya Tunisia uliopangwa kufanyika Machi 27 Jijini Tunis na marudiano Machi 30 Dar es Salaam na Ndayiragije alitaka baada ya mechi hizo mbili za nyumbani na ugenini dhidi ya Tunsia kuwania tiketi ya AFCON, wachezaji wanaocheza nje waruhusiwe kurejea katika klabu zao na wanaocheza nyumbani wabaki kambini kujiandaa na CHAN iliyopangwa kufanyika Cameroon kuanzia Aprili 4 hadi 25, mwaka huu nchini Cameroon.
    Kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa kambini kilikuwa kinaundwa na makipa; Bakari Kissu (Gor Mahia - Kenya), Metacha Mnata (Yanga SC), Aishi Manula (Simba SC) na Salum Salula (Malindi FC).
    Mabeki ni; Shomari Kapombe (Simba SC), Juma Abdul (Yanga SC), Kelvin Kijiri (KMC), Mohamed Hussein (Simba SC), Nickson Kibabage (Difaa Hassan El-Jadidi - Morocco), David Bryson (Gwambina FC), Bakari Nondo (Coastal Unon), Agrey Morris (Azam FC), Kelvin Yondan (Yanga SC), Dickon Job (Mtibwa Sugar), Erasto Nyoni (Simba SC), Said Juma ‘Makapu’ (Yanga SC) na Abdi Banda (Highlands Park FC – Afrika Kusini).
    Viungo ni Jonas Mkude (Simba SC), Himid Mao (ENPPI - Misri), Bryson Raphael (Azam FC), Mapinduzi Balama (Yanga SC), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Hassan Dilunga (Simba SC), Feisal Salum (Yanga SC), Lucas Kikoti (Namungo FC), Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam FC), Farid Mussa (CD Tenerife - Hispania) na Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadidi - Morocco).
    Washambulaji ni; Ayoub Lyanga (Coastal Union), Reliants Lusajo (Namungo FC), Ditram Nchimbi (Yanga SC), John Bocco (Simba SC), Shaaban Iddi Chilunda (Azam FC), Sixtus Sabilo (Polisi Tanzania) na Nahodha Mbwana  Samatta (Aston Villa - England).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDAYIRAGIJE ASEMA ATALAZIMIKA KUUNDA UPYA KIKOSI CHA TAIFA STARS RATIBA MPYA IKITOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top