• HABARI MPYA

  Thursday, March 12, 2020

  KMC YAICHAPA YANGA SC 1-0 NA KUJIINUA KIDOGO KATIKA VITA YA KUEPUKA KUSHUKA DARAJA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU KMC FC ya Kinondoni leo imewaangusha vigogo, Yanga SC baada ya kuwachapa 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Ushindi huo umetokana na bao pekee la mshambuliaji wake, Salimu Aiyee dakika ya 63 akimalizia pasi ya kiungo mshambuliaji Mrundi, Emmanuel Mvuyekure.
  Ushindi huo unaipa ahueni KMC inayopigana vita ya kuepuka kushuka daraja, kwani sasa inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 28 na kupanda had nafasi ya 16, ikiizidi wastani wa mabao tu Mbeya City inashukia nafasi ya 17.


  Yanga SC wenyewe ambao sana wanawania kumaliza nafas ya pili nyuma ya watani wao, Simba SC wanaoelekea kutwaa taji la tatu mfululizo la Ligi Kuu – wanabaki na ponti zao 50 baada ya kucheza mechi 26.
  Kikosi cha KMC kilikuwa; Jonathan Nahimana, Kelvin John, Ally Ramadhani, Ismail Gambo, Sadallah Lipangile, Kenny Ally, Hassan Kabunda/James Msuva dk51, Salimu Aiyee, Mohamed Samatta/Emmanuel Mvuyekule dk50 na Abdul Hilary.
  Yanga SC; Metacha Mnata, Juma Abdul, Adeyum Saleh/Ally Mtoni dk25, Lamine Moro, Said Juma ‘Makapu’, Papy Tshishimbi, Patrick Sibomana/David Molinga dk67, Faisal Salum/Deus Kaseke dk81, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima na Mapinduzi Balama.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAICHAPA YANGA SC 1-0 NA KUJIINUA KIDOGO KATIKA VITA YA KUEPUKA KUSHUKA DARAJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top