• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 12, 2020

  CHIPUKIZI WA TANZANIA, ALLY MSENGI AWAONYESHA KAZI MAMELODI SUNDOWNS LIGI YA AFRIKA KUSINI

  Na Mwandishi Wetu, CAPE TOWN
  KIUNGO chipukizi wa Tanzania, Ally Msengi jana amecheza kwa dakika zote klabu yake, Stellenbosch ikichapwa 1-0 na mabingwa watetezi, Mamelodi Sundowns katika mchezo wa Ligi Kuu Afrika Kusini Uwanja wa 
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Athlone Jijini, Cape Town bao pekee la Mamelodi lilifungwa na Themba Zwane dakika ya tisa.
  Msengi, nyota wa Serengeti Boys na Ngorongoro Heroes aliyejiunga na klabu hio akitokea KMC aliweza kuhimili pambano kwa dakika tisini.
  Ally Msengi wa Stellenbosch akimtoka mchezaji wa Mamelodi Sundowns katika mchezo wa Ligi Kuu Afrika Kusini jana

  Awali alikuwa ameshindwa kucheza tangu asajiliwe mwezi wa kwanza kutokana na kuchelewa  kupata kibali cha kazi.
  Kikosi cha Stellenbosch kilikuwa; Lee Langeveldt, Nyiko Mobbie, Sibusiso Mthethwa, Mogamad De Goede, Marc Van Heerden, Ashley Du Preez/Iqraam Rayners dk60, Granwald Scott/Ryan Moon dk69, Ally Msengi, Leletu Skelem, Ovidy Karuru/ Waseem Isaacs dk79, Asavela Mbekile.
  Mamelodi Sundwons; Denis Onyango, Anele Ngcongca, Motjeka Madisha, Ricardo Nascimento, Tebogo Langerman, Sphelele Mkhulise/Lebohang Maboe dk26, Hlompho Kekana, Andile Jali, Themba Zwane/Jose Meza Draegertt dk73, Sibusiso Vilakazi, Gaston Sirino/Lyle Lakay dk55.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHIPUKIZI WA TANZANIA, ALLY MSENGI AWAONYESHA KAZI MAMELODI SUNDOWNS LIGI YA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top