• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 25, 2020

  ALIYEKUWA AFISA HABARI WA SIMBA SC, ASHA MUHAJI AFARIKI DUNIA LEO HINDU MANDAL

  Na Mwandishi  Wetu, DAR ES SALAAM
  ALIYEWAHI kuwa Afisa Habari wa klabu ya Simba SC, Asha Muhaji amefariki dunia mapema leo katika hosptali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu. 
  Taarifa ya klabu ya Simba leo imesema; “Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyewahi kuwa Msemaji wetu, Asha Muhaji kilichotokea leo katika hospital ya Hindu Mandal Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu,”.
  Naye Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kwamba amezipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Asha Muhaji, kwani alikuwa mmoja wa wana habari wenye mchango mkubwa kwa soka ya nchi hii.
  Buriani Asha Muhaji, umekamilisha yako ya duniani. Tangulia na kapumzike kwa amani. 

  Asha Muhaji aliyewahi kulitumikia shirika la Posta, aliibukia katika magazeti ya Majira na Spoti Starehe mwanzoni mwa miaka ya 1990 kabla ya kuhamia Uhuru na Mzalendo na baadaye Bingwa, Dimba, Mtanzania na Rai kabla ya kuwa Msemaji wa Simba SC wakati wa uongozi wa Alhaj Ismail Aden Rage mwaka 2014.   
  Katika siku za karibuni, Asha pamoja na kuendelea na shughuli zake za Uandishi wa Habari pia alikuwa kwenye kundi la kuhamasisha timu ya timu ya taifa, lijulikanalo kama Taifa Stars Sapota. Mungu amlaze mahali pema peponi Asha. Amin.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ALIYEKUWA AFISA HABARI WA SIMBA SC, ASHA MUHAJI AFARIKI DUNIA LEO HINDU MANDAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top