• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 23, 2020

  HULK AOA MPWA WA MKEWE WA ZAMANI NA KUHAMIA NAYE CHINA

  NYOTA wa Brazil, Hulk ameripotiwa kuoa mpwa wa mke wake zamani, baada ya wawili hao kuweka hadharani mahusiano yao Desemba mwaka jana. 
  Mshambuliaji huyo alihitimisha miaka 12 ya mahusiano na Iran Angelo mwezi Julai mwaka jana kabla ya mahusiano yake na mpw awa mkewe huyo, Camila Angelo kuanikwa baadaye mwaka huo.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amevunja ukimya juu ya mahusiano yake na Camila mwenye umri wa miaka  31 baada ya kuandika ameoa katika wasifu wa ukurasa wake wa mitandao ya jamii.
  Kwa mujibu wa taarifa kutoka gazeti la Infobae laArgentina, ndoa hiyo ilifungwa haraka kutokana na ukweli kwamba Camila alihitaji visa ilia aishi na Hulk huko China. 
  Wawili hao wameposti picha kadhaa wakiwa pamoja ambazo zilonyesha wote wakiwa na pete ya ndoa. 
  Mshambuliaji huyo amefankiwa kupata watoto watatu na Ian, Tiago na Alice na sasa Hulk anashi na Camila China ambako mchezaji huyo anachezea klabu ya Shanghai SIPG FC ya Lig Kuu ya China.  
  Kiungo huyo Mbrazil alikuwa mmoja wa nyota wakubwa waliojiunga na Ligi Kuu ya China mwaka 2016.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HULK AOA MPWA WA MKEWE WA ZAMANI NA KUHAMIA NAYE CHINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top