• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 31, 2020

  MJUMBE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA KLABU YA SIMBA, IDDI MBITA AFARIKI DUNIA LEO ALFAJIRI DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  ALIYEKUWA Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba, Idd Hashimu Mbitta amefariki dunia Alfajiri ya leo Jijini Dar es Salaam.
  “Uongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi, Iddi Mbita kilichotokea leo Alfajiri ya Machi 31, 2020 Jijini Dar es Salaam,” imesema taarifa ya SImba SC leo.
  Naye Mwenyekiti wa Bodi ya klabu ya Simba SC, Mohamed ‘Mo’ Dewji amesema kwamba ameumizwa mno na kifo cha Mbitta kwa sababu wamesoma pamoja shule ya Arusha, wamekuwa marafiki wa muda mrefu.
  “Pumzika kwa amani mpendwa wetu Iddi. Tumesoma pamoja Arusha School, urafiki wetu tukaurithisha hadi kwa watoto wetu kuwa marafiki na sisi kuendelea kufurahia mechi za Simba pamoja. Pumzika kwa amani rafiki yangu, nasi tuko njiani. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un,”amesema Mo Dewji.
  Naye Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Brigedia Hashimu Mbitta kufuata msiba huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MJUMBE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA KLABU YA SIMBA, IDDI MBITA AFARIKI DUNIA LEO ALFAJIRI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top