• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 02, 2020

  KIINGILIO CHA CHINI YANGA NA SIMBA NI SHILINGI 7,000 JUMAPILI YA MACHI 8 UWANJA WA TAIFA

  Na Stella Theopist, DAR ES SALAAM 
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa  Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga na  Simba utakaochezwa Machi 8, mwaka huu.
  Viingilio vya mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa majira ya saa 11 VIP A shilingi 30,000
  VIP B na  C shilingi 15,000 20,000,Viti vya rangi ya Machungwa ni 10,000 Bluu na Kijani shilingi 7,000.
  Tiketi zinapatika katika vituo TCC Club, Imasco/PR,Uwanja wa sabasaba na barabara ya kilwa na Jitegemee kupitia Selcom.
  Hata hivyo shirikisho limewataka watu kuwahi kununua tiketi  mapema kwa kupitia kadi ya Selcom ambayo inakupa urahisi wa kununua tiketi yako.
  Hata hivyo kadi za Selcom zinapatikana kwa mawakala waliopo sehemu mbalimbali nchini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIINGILIO CHA CHINI YANGA NA SIMBA NI SHILINGI 7,000 JUMAPILI YA MACHI 8 UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top