• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 03, 2020

  AZAM FC YAPATA MKUU MPYA WA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO, THABIT ZAKARIA ACHUKUA NAFASI YA JAFFAR IDDI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Azam FC unayofuraha kumtangaza mwandishi mkongwe, Thabith Zakaria 'Zaka Za Kazi', kuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano.
  Zakaria anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaffar Idd, aliyepangiwa majukumu mengine ndani ya kampuni.
  Ujio wa Zakaria ni sehemu ya jitihada za uongozi wa Azam FC kuboresha kitengo cha habari ndani ya timu, ambapo sasa kitatambulika kama Kitengo cha Habari na Mawasiliano kitakachokuwa kikiongozwa naye.
  Tunaamini ya kuwa Zakaria atatumia vilivyo uzoefu mkubwa aliokuwa nao katika tasnia ya habari, alioupata wakati akifanya kazi na makampuni makubwa ya habari ya IPP Media na Azam TV, na kuitangaza vema timu yetu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAPATA MKUU MPYA WA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO, THABIT ZAKARIA ACHUKUA NAFASI YA JAFFAR IDDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top