• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 09, 2020

  VANDENBROECK KOCHA BORA WA MWEZI FEBRUARI WA LIGI KUU, MAYANGA WA NDANDA MCHEZAJI BORA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Simba SC, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2019 – 2020.
  Vandenbroeck aliye katika msimu wake wa kwanza SImba SC tangu arithi mikoba ya Mbelgiji mwenzake, Patrick Aussems ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Mrundi Hitimana Thierry wa Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi na Abdul Mingange wa Ndanda SC ya Mtwara.
  Aidha, mshambuliaji Vitalis Mayanga wa Ndanda SC amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu baada ya kuwashinda Reliants Lusajo na Blaize Bigirimana wote wa Namungo alioingia nao fainali.
  Katika mwezi Februari, Simba SC imecheza mechi saba, imeshinda sita 2-0 dhidi ya Coastal Union, 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, 1-0 dhidi ya Lipuli FC, 1-0 dhidi ya Kagera Sugar na 3-1 dhidi ya Biashara United na kufungwa moja dhidi ya JKT Tanzania 1-0.
  Mabingwa hao watetezi, Simba SC wanaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa mbali, wakiwa na pointi 68, wakifuatiwa na Azam FC yenye pointi 51 baada ya wote kucheza mechi 27, wakati Yanga ni ya tatu kwa pointi zake 50 za mechi 25.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VANDENBROECK KOCHA BORA WA MWEZI FEBRUARI WA LIGI KUU, MAYANGA WA NDANDA MCHEZAJI BORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top