• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 05, 2020

  MARTIN SAANYA KUCHEZESHA MECHI YA SIMBA NA YANGA MBELE YA RAIS WA CAF, AHMAD JUMAPILI

  Na Stella Theopist, DAR ES SALAAM 
  REFA Martin Saanya wa Morogoro ndiye atakayepuliza kipyenga katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Yanga SC na Simba itakayohudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Jumapili Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 
  Katika mchezo huo namba 260  Saanya atasaidia wa mwamuzi Namba Moja (Line One) Mohamed Mkono Kutoka Tanga, Mwamuzi Namba Mbili (Line Two) Frank Komba wa Dar es Salaam, pia  Mwamuzi wa Mezani (Fourth Official) Elly Sasii wa Dar es Salaam.
  Hali hii imekuja baada kuwa na malalamiko mengi  juu ya waamuzi na kuhakikisha mchezo huo unachezeshwa kwa ubora na kutangaza waamuzi wawili wa ziada ambao watasimama kwenye mstari wa goli  ambao Ni Abdallah Mwinyimkuu wa Singida Na Ramadhani Kayoko wa Daresalaam.
  Mtathimini wa  waamuzi katika mechi hiyo atakuwa Ni Sudi Abdi wa Arusha na Kamishina wa mchezo Ni Mohamed Mkweche wa Dar es Salaam.
  Hata hivyo mara ya kwanza  Tanzania Kutumia muundo huu was waamuzi ilikuwa Ni mwaka 2019 wakati wa mechi za hatua ya robo Fainali ya Michuano ya Afcon U17 iliyofanyika jijini Daresalaam.
  Hata hivyo Mchezo huu wa jumapili unatarajiwa kuhudhuliwa na Rais wa CAF Ahmad Ahmad ambaye pia atakuwa Ni mgeni wa Heshima siku hiyo ya mechi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MARTIN SAANYA KUCHEZESHA MECHI YA SIMBA NA YANGA MBELE YA RAIS WA CAF, AHMAD JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top