• HABARI MPYA

  Jumapili, Machi 22, 2020

  RAIS WA ZAMANI WA REAL MADRID AFARIKI KWA UGONJWA WA CORONA

  RAIS wa zamani wa Real Madrid, Lorenzo Sanz amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 76 baada ya kukutwa na virusi vya corona.
  Sanz alikuwa Mkurugenzi Real kuanzia mwaka 1985 hadi 1995 kabla ya kuwa Rais wa klabu, wadhifa aliodumu nao hadi mwaka 2000.
  Ndiye aliyetengeneza mkakati madhubut wa kutwaa Kombe la Ulaya mwaka 1998, wakiifunga Juventus kwenye fainali na kumaliza ukame wa miaka 32 wa taji hilo na kutawala tena.
  Baada ya kubeba La Septima wakaongeza miaka mingine miwili baadaye mwaka 2000. Pia aliwanunua Davor Suker, Roberto Carlos na Nicholas Anelka wakatua Bernabeu.
  Rais wa zamani wa Real Madrid, Lorenzo Sanz amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 76 

  Mtoto wa Sanz, Lorenzo San Duran ameandika kwa uchungu kwenye Twitter: "Baba yangu amefariki dunia ,".
  "Hakustahili mwisho kama huu. Mmoja kati ya bora, mtu jasri na mchapakazi niliyemuona maishani mwangu. Shauku yake ilikuwa ni familia yake na Real Madrid,". 
  Ushindi wa mwaka 1998 ulikuwa wa kwanza wa taji hilo la Ulaya kwa Real tangu mwaka 1966. Rais aliyemfuatia Real ni Florentino Perez, ambaye aliendeleza zama za Galactico na akarejea mwaka 2009.
  Sanz aliinunua Malaga mwaka 2006 kabla ya kuiuza 2010.
  Alikuwa baba mkwe wa beki wa zamani wa Real Madrid, Michel Salgado, ambaye alimuoa binti wa Sanz, Malula.
  Mtoto wa Sanz, Fernando aliichezea Real kati ya 1996 na 1999. Mungu ampumzishe kwa amani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAIS WA ZAMANI WA REAL MADRID AFARIKI KWA UGONJWA WA CORONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top