• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 10, 2020

  NDAYIRAGIJE AMREJESHA MAKAPU TAIFA STARS, AMUITA NA KAPOMBE KUIVAA TUNISIA KUFUZU AFCON

  Na Stella Theopist, DAR ES SALAAM 
  KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Mrundi Etienne Ndayiragije amemrejesha kikosini kiungo Said Juma ‘Makapu’ wa Yanga SC, ingawa safari hivi hii ameitwa katika kundi la walinzi.
  Na hiyo ni baada ya kijana huyo kufanya vizuri Yanga SC hivi karibuni akichezeshwa kama mlinzi wa kati chini ya kocha Mbelgiji, Luc Eymael kufuatia miaka mitatu ya kupoteza nafasi kuanza kikosi cha kwanza cha klabu yake hadi Taifa Stars.
  Katika kikosi chake wachezaji 35 kinachotarajiwa kuingia kambini keshokutwa kujiandaa na mchezo wa Kundi J kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Tunisia Machi 27 Jijini Tunis na kurudiana Dar es Salaam Machi 30, Ndayiragije pia amemuta beki wa kulia wa Simba SC, Shomari Kapombe.
  John Bocco (kushoto) na Said Juma 'Makapu' wote wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars

  Kapombe aliomba kutoitwa Taifa Stars ili aelekeze nguvu zake kwenye klabu yake, akidai kwamba hayuko fiti kiasi cha kuweza kutumika kote kote.
  Ndayiragije amesema kikosi hicho cha wachezaji 35 baada ya mchezo wa nyumbani na ugenini kuwania tiketi ya AFCON wachezaji wanaocheza nje wataruhusiwa kurejea katika klabu zao na wanaocheza nyumbani wataingia kambini kujiandaa na Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zitakazofanyika Cameroon kuanzia Aprili 4 hadi 25, mwaka huu nchini Cameroon
  Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichotajwa leo kinaundwa na makipa; Bakari Kissu (Gor Mahia - Kenya), Metacha Mnata (Yanga SC), Aishi Manula (Simba SC) na Salum Salula (Malindi FC).
  Mabeki ni; Shomari Kapombe (Simba SC), Juma Abdul (Yanga SC), Kelvin Kijiri (KMC), Mohamed Hussein (Simba SC), Nickson Kibabage (Difaa Hassan El-Jadidi - Morocco), David Bryson (Gwambina FC), Bakari Nondo (Coastal Unon), Agrey Morris (Azam FC), Kelvin Yondan (Yanga SC), Dickon Job (Mtibwa Sugar), Erasto Nyoni (Simba SC), Said Juma ‘Makapu’ (Yanga SC) na Abdi Banda (Highlands Park FC – Afrika Kusini).
  Viungo ni Jonas Mkude (Simba SC), Himid Mao (ENPPI - Misri), Bryson Raphael (Azam FC), Mapinduzi Balama (Yanga SC), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Hassan Dilunga (Simba SC), Feisal Salum (Yanga SC), Lucas Kikoti (Namungo FC), Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam FC), Farid Mussa (CD Tenerife - Hispania) na Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadidi - Morocco).
  Washambulaji ni; Ayoub Lyanga (Coastal Union), Reliants Lusajo (Namungo FC), Ditram Nchimbi (Yanga SC), John Bocco (Simba SC), Shaaban Iddi Chilunda (Azam FC), Sixtus Sabilo (Polisi Tanzania) na Nahodha Mbwana  Samatta (Aston Villa - England).
  Ndayiragije amesema wachezajj wa Yanga watachelewa kuingia kambini kwa sababu wameruhusiwa kuichezwa klabu yao mechi ya kiporo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Namungo Jumapili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NDAYIRAGIJE AMREJESHA MAKAPU TAIFA STARS, AMUITA NA KAPOMBE KUIVAA TUNISIA KUFUZU AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top