• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 18, 2020

  HAJAMSAHAU ‘MAMA WATOTO’, MAYWEATHER AFIWA NA MJOMBA

  BONDIA Floyd Mayweather amepata pigo baada ya kufiwa na mjomba wake, Roger Mayweather aliyetoa mchango mkubwa katika mafanikio yake ya ulingoni.
  Roger Mayweather amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 58 kufuatia kusumbuliwa kwa muda na ugonjwa wa sukari.
  Roger Mayweather pa ni bondia wa zamani aliyestaafu mwaka 1999, kabla ya kuwa kocha wa Floyd Mayweather.
  Hili ni pigo lingine kwa ‘Mtu Pesa’ kufuatia mama wa watoto wake watatu, Josie Harris kukutwa na Polisi amekufa kwenye gari yake Jijini California wiki iliyopita.

  Licha ya wawili hao kutengana, bondia huyo mwenye umri wa miaka 43 siku za karibuni amekuwa akiposti picha akiwa na Harris kwenye Instagram enzi zao za furaha. 
  Picha hizo aliziambatanisha maelezo ya kumuenzi, akimuita 'mwamba wangu' 'rafiki yangu', 'malaika wangu na 'mpenzi wangu'. 
  Roger alikuwa mwalimu mkuu wa Floyd mwenye rekodi ya kushinda mapambano yake yote 50 alipojiunga na ngumi za kulipwa mwaka 1996 hadi baba yake, Floyd Mkubwa alipotoka jela miaka miwili baadaye.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HAJAMSAHAU ‘MAMA WATOTO’, MAYWEATHER AFIWA NA MJOMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top