• HABARI MPYA

  Friday, March 13, 2020

  AZAM FC YAMPA MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI KIUNGO WAKE MKABAJI, MUDATHIR YAHYA ABBAS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imeingia mkataba mpya wa miaka miwili na kiungo wake mkabaji, Mudathir Yahya Abbas.
  Mkataba wa awali wa kiungo huyo ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo kwa kusaini mkataba mpya, kutamfanya aendelee kusalia kwenye viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2022.
  Mudathir amekuwa na kiwango bora kwenye eneo la ukabaji tokea ajiunge na Azam Academy mwaka 2011, hadi kupandishwa timu kubwa miaka minne iliyopita.
  Msimu huu amefanikiwa kuifungia bao moja Azam FC, kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMPA MKATABA MPYA WA MIAKA MIWILI KIUNGO WAKE MKABAJI, MUDATHIR YAHYA ABBAS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top