• HABARI MPYA

  Tuesday, March 24, 2020

  MEXIME ASITA KUHAMIA YANGA SC, ASEMA ANATEMBEA NA MKATABA WAO TANGU MWAKA JANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Kagera Sugar Mecky Mexime amefichua kwa mara ya kwanza kuwa anatakiwa na klabu ya Yanga ameshapewa mkataba huo tangu mwishoni mwa mwaka jana, lakini kuna baadhi ya vipengele havijakaa sawa hivyo bado hajasaini mkataba huo wala kuurudisha.
  Mexime beki na Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Tafa Stars amesema kwamba kuzifundisha timu za Simba, Yanga au Azam ni rahisi sana kuliko vilabu vingine vya Tanzania. 
  Inaaminika, Mwenyekiti wa Yanga SC, Dk. Mshindo Msolla ni shabiki mkubwa wa Mexime tangu anacheza nafasi za ulinzi klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  Na Msolla ndiye anayemtaka zaidi Mexime akawe Kocha Msaidizi wa Yanga SC, ambayo kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu Mbelgiji, Luc Eymael anayesadiwa na mzalendo, Charles Boniface Mkwasa.
  Yanga ilitaka kumpandisha Mkwasa hadi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, lakini ikazimika kumfanya Msaidizi wa Eymael kutokana na Mexime kusita kusaini mkataba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MEXIME ASITA KUHAMIA YANGA SC, ASEMA ANATEMBEA NA MKATABA WAO TANGU MWAKA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top